Thursday 24 November 2016

RAIS MALINZI ALIZWA NA MSIBA MWINGINE YOUNG AFRICANS

“Nimeshtushwa,” ni neno moja tu la Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi mara baada ya kupata taarifa za kifo cha Hamad Kiluvia ambaye ni mmoja wa viongozi wa Young Africans Sports Club. 

Hamad Kilivua amefariki dunia leo alfajiri Novemba 23, 2016 jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku ambayo Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Isaac Shekiondo ‘Clinton’ amezikwa kwao Korogwe mkoani Tanga. 

Kilichomshitua Rais Malinzi ni kifo cha Kiluvia akisema kinakwenda sambamba na cha Shekiondo aliyefariki dunia Novemba 20, mwaka huu kwenye Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam. 

Leo amepata taarifa za kifo cha Kiluvia ambaye alikuwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Young Africans. Enzi za uhai wake, Kiluvia akiwa Mjumbe wa bodi hiyo alishirikiana na Malinzi wakati huo wakiwa viongozi wa juu wa Klabu hiyo ambayo Makuu yake yako kwenye makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga, Kariakoo, Dar es Salaam. 

Rais Malinzi amesema amepokea kwa masikitiko kifo cha Kiluvia kwa kuwa anafahamu vema utendaji wakati huo akiwa Kiongozi wa Young Africans Sports Club. Alikuwa ni mtu mpole, mwenye kusikiliza na kutatua changamoto za klabu aliyependa mpira wa miguu na kutoa misaada na fedha na mawazo kadiri ya uwezo wake. 

Kadhalika Rais Malinzi alituma salamu hizo kwa familia ya marehemu Kiluvia ndugu, jamaa na marafiki ambayo kwa muda walikuwa wakimuuguza mpendwa wao na hivyo kutokana na kifo hicho, amewataka kuwa watulivu kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao. 

Msiba wa Kiluvia uko nyumbani kwake, Mikocheni Regent Estate jirani na Ofisi za Baraza la Mazingira (NEMC) ambako taratibu za mazishi zinafanyika. 

RAUNDI YA PILI AZAM SPORTS FEDERATION CUP 2016/2017

Wakati Baruti ya Mara ikiifunga Ambassador ya Simiyu mabao 3-1 katika mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), ndani ya Uwanja wa Halmashauri Kahama, michezo mingine inatarajiwa kuendelea Novemba 27, mwaka huu kwenye viwanja mbalimbali kwa mujibu wa ratiba.

Hatua ya pili itakutanisha timu zlizopenya hatua ya kwanza iliyofanyika wikiendi iliyopita. Mechi zinazotarajiwa kucheza hatua inayofuata ni Tomato dhidi ya Jangwani katika mchezo utakaofanyika mkoani Njombe.
 
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA