Saturday 3 December 2016

DONALD TRUMP AMTEUA JENERALI JAMES MATTIS KUWA WAZIRI WA ULINZI



Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteuwa Jenerali James Mattis, ambaye aliwahikuwa mwanajeshi wa kikosi cha majini nchini Irak na Afghanistan, kuwa Waziri wa Ulinzi.

Jenerali Mattis ambaye anajulikana pia kama “Mad Dog” alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa rais Barack Obama, kuhusiana na sera za Mashariki ya Kati, hususan kuhusiana na nchi ya Iran.

Jenerali Mattis amekuwa akielezea Iran kama kama taifa pekee tishio kwa amani na utulivu wa mataifa ya Mashariki ya Kati.
Donald Trump akimnyooshea kidole Jenerali Mattis kati kati akiwa na Makamu wa rais Mteule Mike Pence

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA