Showing posts with label uteuzi. Show all posts
Showing posts with label uteuzi. Show all posts

Tuesday, 6 June 2017

RAIS MAGUFULI AMUAPISHA BI.ANNA MGHWIRA KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Juni, 2017 amemuapisha Bi. Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Bi. Anna Elisha Mghwira amejaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Hafla ya kuapishwa kwa Bibi Anna Elisha Mghwira imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Akizungumza baada ya kumuapisha, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Bi. Anna Elisha Mghwira kwenda kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuondoa kero zinazowakabili wananchi wa Kilimanjaro bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa, dini, makabilia na kanda wanazotoka.

Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa atapata ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake na asikubali kuyumbishwa na mtu yeyote katika majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.

“Mimi huwa siteui watu hivi hivi, huwa naangalia uwezo wa mtu, na wewe nimekuchunguza na nimejiridhisha kuwa una uwezo wa kuwatumikia wananchi, nenda kachape kazi, kawaondolee kero wananchi wa Kilimanjaro, wapo watu watakaokusema na wengine watakuonea wivu, wewe kachape kazi” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Bi.Anna Elisha Mghwira amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na amemuahidi kuwa yupo tayari kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kujenga Taifa.

“Ninasema hii ni heshima kwa Taifa letu, ni heshima kwa umoja wa nchi yetu, ni heshima kwa siasa za umoja wa nchi yetu, kumekuwa na minong’ono mingi sana kuwa Rais analeta nini, kuteua watu wanaitwa wapinzani, mimi sio mpinzani wa maendeleo” amesema Bi. Mghwira. 


Sunday, 12 February 2017

RAIS MAGUFULI AWAPANGIA VITUO VYA KAZI MABALOZI WATATU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wapya watatu ambao aliwateua tarehe 03  Desemba 2016.
 
Mabalozi hao waliopangiwa vituo ni Joseph Sokoine anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Omar Yussuf Mzee anayekuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Algeria na Grace Mgavano anayekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladis Komba nchini Uganda ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
 
Aidha, Balozi Sokoine ambaye anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Deodorus Kamala ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
 
Balozi Mzee kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alishawahi kushika nafasi mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na nafasi ya mwisho alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya kwanza ya Rais Dkt. Ali Mohammed Shein.
 
Kwa upande wa Balozi Mgavano kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Ubalozi alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu.
 
Mabalozi wote waliopangiwa vituo vya kazi wataapishwa na Rais Ikulu jijini Dar Es Salaam leo  Jumapili tarehe 12 Februari 2017 saa tano asubuhi.

Friday, 27 January 2017

MKUU WA WILAYA UYUI AJIUZULU, AMWANDIKIA BARUA RAIS DKT MAGUFULI


Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.

Akieleza sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea kusongwa na majukumu binafsi.

Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.

Tuesday, 17 January 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WABUNGE WAWILI NA BALOZI MMOJA.

Image result for bunge la tanzania


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.

Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Abdallah Bulembo ndiye mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na pia alikuwa ni mujumbe wa Bunge Maalum la Katiba, kabla ya majukumu ya kuendesha kampeni za urais mwaka 2015 zilizomuingiza Rais Magufuli madarakani.

Kwa upande wake Prof Kabudi, ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria, lakini kilichong'arisha zaidi ni pale alipoteuliwa na Rais Kikwete kuwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Katiba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba.

Prof. Kabudi amekuwa mahiri katika mihadhara mbalimbali kitaifa, hasa wakati ule wa mchakato wa Katiba Mpya.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa

Saturday, 10 December 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI PIA AKUTANA NA MMILIKI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE KILICHOPO MTWARA ALHAJI ALIKO DANGOTE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Displaying 1.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 2-mtigumwe.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 3-Sasabo.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambaye atakuwa katika upande wa (Mawasilino), Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 4.Aloyce.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 5.jpg
Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole-Sendeka.
Displaying 5.G.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 6.jpg
Viongozi walioapishwa waki weka saini katika viapo vya maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka.

Displaying 7..jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na viongozi walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe, Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka, Wakwanza kutoka kulia ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin pamoja na Katibu Mkuu wa Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo.

Displaying 8..jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 9.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha pamoja na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 10.jpg

Displaying 11.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kumaliza kwa kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 13.jpg
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Displaying 14.jpg
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Displaying 15.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza kikao chake na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam.
Displaying 16.jpg

Displaying 17.jpg


Displaying 18.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Saturday, 3 December 2016

DONALD TRUMP AMTEUA JENERALI JAMES MATTIS KUWA WAZIRI WA ULINZI



Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteuwa Jenerali James Mattis, ambaye aliwahikuwa mwanajeshi wa kikosi cha majini nchini Irak na Afghanistan, kuwa Waziri wa Ulinzi.

Jenerali Mattis ambaye anajulikana pia kama “Mad Dog” alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa rais Barack Obama, kuhusiana na sera za Mashariki ya Kati, hususan kuhusiana na nchi ya Iran.

Jenerali Mattis amekuwa akielezea Iran kama kama taifa pekee tishio kwa amani na utulivu wa mataifa ya Mashariki ya Kati.
Donald Trump akimnyooshea kidole Jenerali Mattis kati kati akiwa na Makamu wa rais Mteule Mike Pence

Tuesday, 22 November 2016

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA KATIBU TAWALA WA MKOA WA KAGERA (RAS) KAMISHNA DIWANI ATHUMANI LEO IKULU DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Kamishna Diwani Athumani baada ya kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Katibu wa Maadili ya Viongozi – Siasa, Bw. Waziri Kipacha akimuongoza Kamishna Diwani Athumani kula kiapo cha uadilifu cha viongozi wa umma baada ya kuapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Kamishna Diwani Athumani pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama umma baada ya Kamishna Diwani kuapishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.

PICHA NA IKULU 

Monday, 21 November 2016

RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TRA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 20 Novemba, 2016 amemteua Bw. Charles E. Kichere kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Bw. Charles E. Kichere anajaza nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA iliyokuwa wazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uteuzi huu umeanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Sunday, 20 November 2016

Tuesday, 18 October 2016

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA AJALI YA BASI LA BARCELONA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi kufuatia vifo vya watu 11 vilivyosababishwa na ajali ya basi la kampuni ya Barcelona iliyotokea jana tarehe 17 Oktoba, 2016 katika eneo la Miteja Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi.

Basi hilo lenye namba T 101 CUU lililokuwa likisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kijiji cha Mahuta katika Wilaya ya Newala Mkoani Lindi, lilipinduka baada ya gurudumu lake la kushoto kupasuka na kusababisha vifo vya watu 10 papo hapo na mwingine 1 kufariki dunia baadaye akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Lindi, huku watu wengine 43 wakiwa wamejeruhiwa.

Katika salamu zake, Rais Magufuli amesema amepokea taarifa za vifo vya watu hao kwa mshituko na huzuni kwa kuwa kwa mara nyingine Taifa limepoteza watu wake na familia zimepoteza wapendwa wao na watu ambao ziliwapenda na kuwategemea.

"Ndugu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Godfrey Zambi naomba unifikishie salamu nyingi za pole kwa wote waliopoteza jamaa na ndugu zao katika ajali hii, kwa hakika nimeguswa sana na vifo hivi na naungana na familia za marehemu wote katika maombolezo na sala" amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amewasihi wote walioguswa na vifo hivyo kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi na amewaombea Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Pia Rais Magufuli amewaombea majeruhi wote wapone haraka ili waungane na familia zao na kurejea katika shughuli za ujenzi wa Taifa,
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Oktoba, 2016.

Monday, 3 October 2016

RAIS MAGUFULIJP AMTEUA PROF. LAWRENCE MUJUNGU MUSERU KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

03 Oktoba, 2016

Monday, 22 August 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA GABRIEL DAQARRO KUWA MRITHI WA GAMBO ARUSHA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Agosti, 2016 amemteua Bw. Gabriel Fabian Daqarro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Bw. Gabriel Fabian Daqarro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Mrisho Mashaka Gambo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Uteuzi wa Bw. Gabriel Fabian Daqarro unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
21 Agosti, 2016

Saturday, 16 July 2016

AMEKUMBUKWA::AUGUSTINO LYATONGA MREMA ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA TAIFA YA PAROLE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyopewa amefanya uteuzi wa viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali, na pia amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
  1. Augustino Lyatonga Mrema.
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole kwa kipindi cha miaka mitatu, kuanzia leo tarehe 16 Julai, 2016.
  • Augustino Lyatonga Mrema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Mhe. Eusebia Nicholaus Munuo ambaye muda wake umemalizika.
  1. William R. Mahalu
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
  1. Mohamed Janabi
  • Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Angelo Mtitu Mapunda
  • Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Sengiro Mulebya
  • Ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Oliva Joseph Mhaiki
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Winifrida Gaspar Rutaindurwa
  • Ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC). Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
  1. Charles Rukiko Majinge
  • Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Uteuzi huu umeanza leo tarehe 16 Julai, 2016.
  1. Julius David Mwaiselage
  • Ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.

Kupandishwa Vyeo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa 25 wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1. Essaka Ndege Mugasa
  2. Adamson Afwilile Mponi
  3. Charles Ndalahwa Julius Kenyela
  4. Richard Malika Revocatus
  5. Geofrey Yesaya Kamwela
  6. Lucas John Mkondya
  7. John Mondoka Gudaba
  8. Matanga Renatus Mbushi
  9. Frasser Rweyemamu Kashai
  10. Ferdinand Elias Mtui
  11. Germanus Yotham Muhume
  12. Fulgence Clemence Ngonyani
  13. Modestus Gasper Lyimo
  14. Mboje John Shadrack Kanga
  15. Gabriel G.A. Njau
  16. Ahmed Zahor Msangi
  17. Anthony Jonas Rutashubulugukwa
  18. Dhahir Athuman Kidavashari
  19. Ndalo Nicholus Shihango
  20. Shaaban Mrai Hiki
  21. Simon Thomas Chillery
  22. Leonard Lwabuzara Paul
  23. Ahmada Abdalla Khamis
  24. Aziz Juma Mohamed
  25. Juma Yussuf Ally

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Polisi wengine 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Waliopandishwa vyeo hivyo ni kama ifuatavyo;

  1. Fortunatus Media Musilimu
  2. Goyayi Mabula Goyayi
  3. Gabriel Joseph Mukungu
  4. Ally Omary Ally
  5. Edward Selestine Bukombe
  6. Sifael Anase Mkonyi
  7. Naftari J. Mantamba
  8. Onesmo Manase Lyanga
  9. Paul Tresphory Kasabago
  10. Dadid Mshahara Hiza
  11. Robert Mayala
  12. Lazaro Benedict Mambosasa
  13. Camilius M. Wambura
  14. Mihayo Kagoro Msikhela
  15. Ramadhani Athumani Mungi
  16. Henry Mwaibambe Sikoki
  17. Renata Michael Mzinga
  18. Suzan Salome Kaganda
  19. Neema M. Mwanga
  20. Mponjoli Lotson
  21. Benedict Michael Wakulyamba
  22. Wilbroad William Mtafungwa
  23. Gemini Sebastian Mushi
  24. Peter Charles Kakamba
  25. Ramadhan Ng’anzi Hassan
  26. Christopher Cyprian Fuime
  27. Charles Philip Ulaya
  28. Gilles Bilabaye Muroto
  29. Mwamini Marco Lwantale
  30. Allute Yusufu Makita
  31. Kheriyangu Mgeni Khamis
  32. Nassor Ali Mohammed
  33. Salehe Mohamed Salehe
  34. Mohamed Sheikhan Mohamed
Maafisa hawa wa Jeshi la Polisi Tanzania wamepandishwa vyeo kuanzia tarehe 15 Julai, 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Julai, 2016

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA