Sunday 4 December 2016

SIMANZI::MSHAMBULIAJI UNDER 20 MBAO FC AFARIKI DUNIA UWANJANI,ALIKUWA MWANAFUNZI WA MWANZA SECONDARY

Ismail Mrisho Khalfan akipelekwa kwenye gari baada ya kuanguka uwanjani ili akimbizwe hospitali PICHA ZOTE NA FAUSTINE RUTTA


MSHAMBULIAJI wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Mbao FC ya Mwanza, Ismail Mrisho Khalfan amefariki dunia leo mjini Bukoba baada ya kuanguka uwanjani.

Mchezaji huyo alianguka Uwanja wa Kaitaba, Bukoba dakika chache baada ya kuifungia bao timu yae katika ushindi wa 2-0 kufuatia kugongana na mchezaji wa Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vijana Tanzania Bara.

Baada ya kuanguka alipatiwa huduma ya kwanza na kuonekana hali yake si ya kawaida, hivyo kukimbizwa hospitali ya mkoa wa Kagera kwa matibabu zaidi, ambako umauti ulimfika na tayari imethibitishwa na daktari wa hospitali ya rufaa ya Bukoba kuwa, amefariki dunia na mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.


Ismail Mrisho Khalfan akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka uwanjani ili akimbizwe hospitali


“Alianguka uwanjani ghafla baada ya kufanyiwa faulo mguuni akainama kushika mguu tukamuona ameshika kifua akaanguka chini lakini wakati anaanguka alikuwa peke yake”, ni maneno ya manager wa Mbao FC Bashiri wakati akizungumza na kituo kimoja cha radio cha mkoani Dar es Salaam.
“Tukajaribu kumsaidia kumpatia huduma madaktari wa timu zote pamoja na msalaba mwekundu tukasaidiana kumpeleka hospitali.”
“Wakati huo timu yetu ilikuwa ikiongoza kwa goli 1-0 goli lililofungwa na marehem Ismail Khalfan na jingine lilifungwa wakati mimi sipo nikiwa nimeenda hospitali.”

Mchezaji huyo amefariki akiwa ana umri wa miaka 19 na akiwa ametoka tu kufanya mtihani wa kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya Mwanza, maarufu 'Mwanza Seco'.

Gari lililombeba Ismail Mrisho Khalfan likielekea hospitali 

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA