Monday 13 March 2017

HAWA NDIO WANACHAMA WA UKAWA WALIOJIUNGA NA CCM

Wakati Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ulipokuwa ukiendelea mkoani Dodoma, baadhi ya waliokuwa wachama na viongozi wa ngazi za juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT-Wazalendo wamepokelewa rasmi na CCM baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.

Viongozi hao waliojiunga na CCM wamesema sababu kubwa iliyopelekea na kufikia uamuzi huo ni utendaji kazi wa Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli.

Miongoni mwa wengi waliopokelewa ni pamoja na, Moses Machali Mbunge wa zamani wa Kasulu Mjini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi na baadae kuahimia ACT Wazalendo.

Machali alitangaza kujiunga CCM Novemba mwaka jana ambapo leo amepokelewa rasmi. Dkt Yared Fubusa, Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Mkoa wa Kigoma na Mgombea Ubunge jimbo Kigoma Kaskazini (CHADEMA).

Mwingine ni aliyetangaza kujiunga na CCM na kupokelewa na Mkutano Mkuu ni, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Said Arfi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA