Thursday, 28 September 2017

ASILIMIA 75% YA NCHI WANACHAMA WA INTERPOL, YAKUBALI KUJIUNGA KWA PALESTINA KATIKA TAASISI HIYO

Mwakilishi wa Palestina akipokea bendera kutoka kwa Rais wa Interpol Bw. Meng Hongwei kuashiria uanachama kamili wa Palestina ndani ya Taasisi ya Polisi ya Kimataifa ya kuzuia uhalifu wa kijinai duniani.


Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Polisi wa kimataifa wa kuzuia uhalifu wa kijinai “Interpol”, umekubali kujiunga kwa Palestina katika taasisi hiyo,baada ya nchi wanachama 75 kulipigia kura ya ndio azimio hilo. Interpol imethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa, Palestina na visiwa vya Solomon kuanzia sasa ni miongoni mwa wanachama wake.

Interpol ni taasisi kubwa zaidi ya kipolisi wa kimataifa iliyoasisiwa mwaka 1923, inajumuisha masuala ya nchi wanachama 190,huku makao makuu yake yakiwa mjini Lyon nchini Ufaransa.Aidha Interpol imekubali uanachama wa Palestina mnamo siku ya jumatatu iliyopita jioni kufuatia ombi la nchi hiyo, kabla ya kulijumuisha katika ajenda zake zitakazopigiwa kura katika Mkutano wake Mkuu,ambao uliketi nchini China Jumatano iliyopita na kuikubalia Palestina ombi lake hilo.

Kwa upande mwingine,Israeli na Marekani zilijaribu kukwamisha hatua hiyo ya kukubaliwa uanachama wa Palestina katika Interpol, kwa kutumia mashinikizo kadhaa juu ya taasisi hiyo ili isikubali ombi la Palestina kuwa mwanachama.

Wakati huo huo, Dr.Riyad Al-Maliki ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina, amepongeza hatua ya kuipigia kura ya ndio nchi yake na hatimae kukubaliwa uanachama wa Interpol,kupitia mkutano wake mkuu uliofanyika mjini Beijing nchini China. Amesisitiza kuwa hatua hiyo inathibitisha kuaminika uwezo wa Palestina katika kutekeleza sheria,dhamira halisi na maadili muhimu ya Interpol.

Waziri pia ameashiria kupatikana kwa ushindi huo,kumetokana na msimamo wa awali wa idadi kubwa ya nchi wanachama wa Interpol, iliyotetea sababu ya kuwepo kwa taasisi hiyo na kanuni zake za msingi,pale zilipokataa waziwazi kuupa nafasi ubabe wa kisiasa utawale. Huku waziri akiongeza kusema:"Leo haki na kanuni zimeshinda mambo mengine yote"."Leo, ukweli na kanuni zimeshinda mambo mengine yote.

Dr.Riyad Al-Maliki kwa niaba ya taifa la Palestina,amezishukuru nchi wanachama zilizoiunga mkono Palestina katika jitihada zake,huku akitilia mkazo kuendelea kwa nchi yake katika jitihada za kujiongezea hadhi na nafasi mbalimbali kimataifa,ikiwa ni pamoja na kutetea haki za Wapalestina,uhuru na amani yao kwa njia ya kidiplomasia na kisheria, ikiwa ni pamoja na kujiunga na taasisi husika za kimataifa.

Kwa mnasaba huu pia, Waziri Al-Maliki amesisitiza ahadi ya nchi yake ya Palestina katika kutimiza majukumu yake ya kuchangia kupambana na uhalifu na kuimarisha utawala wa sheria katika ngazi ya kimataifa. Huku ikishirikiana na nchi wanachama wa Interpol katika kukuza hadhi na nafasi ya taasisi hiyo, ushiriki wa kidhati kabisa wa kimataifa dhidi ya uhalifu unaohatarisha maisha wananchi na mustakabali wao duniani.

Aidha ameongeza kusema: "Nchi ya Palestina inauchukulia uanachama huu na majukumu yake kama ni sehemu ya wajibu wake kwa Wapalestina,pia ni wajibu wa kimaadili kwa walimwengu wote. Palestina ipo tayari na inaweza kubeba majukumu na wajibu huu kama mshirika wa dhati katika jamii ya kimataifa,itachangia hasa kuendeleza maadili yetu ya msingi ya pamoja kama mataifa. "

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA