Thursday, 28 September 2017

MISA TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA UTAFITI KUHUSU UWAZI KWENYE TASSISI ZA UMMA

Wadau wa habari nchini wameomba kupata taarifa iwe ni haki ya kila mtu ambayo inapaswa kulindwa kwa nguvu  zote na ni kiashiria kimoja wapo cha serikali yenye uwazi na inayothamini mchango na ushiriki wa wananchi wake katika ujenzi wa taifa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, wamesema kila mtu ana haki ya kupokea na kutoa taarifa ili mradi tu asiende nje ya swala husika.
Wamesema kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya haki ya kila mtu na kupata taarifa muhimu kwa Maisha yao ikiwa ndani ya hifadhi ya Serikali na kwingineko, namna viongozi waliyochaguliwa na wanavyotekeleza majukumu yao.
Katika maadhimisho hayo MISA-TAN walikabidhi tuzo kwa taasisi mbali mbali za umma zinazotoa taarifa kwa uwazi na zile zinazobana taarifa. Kwa mwaka 2017, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa kwanza kwa utoaji na upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma na taasisi iliyokuwa mshindi wa mwisho ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada ya kubainika kuwa inabana taarifa.  Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kila Mtanzania Anayo Haki Ya Kupewa Taarifa."



Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania. Bi. Lianne Houben akizungumzia jinsi ubalozi unavyofanya kazi na taasisi za habari hapa nchini ili kuweza kufanikisha upatikanaji wa habari kwa wananchi nchini Tanzania.

Mgeni Rasmi Jaji Mstaafu na Mwenyekiti aliyepita wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala,   Amiri Ramadhani Manento, akifungua maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akizungumza akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kauli mbiu ya mwaka huu "Kila Mtanzania anayo haki ya Kupewa Taarifa" 
Makamu Mwenyekiti wa MISA Tanzania, WakiliJames Malenga akizungumzia vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
 Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart( wa pili kutoka kulia) pamoja na wadau mbalimbali wakiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa Chapisho la Upatikanaji Taarifa kwa taasisi za umma kwa mwaka 2017.
  Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart  akionesha kufuli la Dhahabu lililokwenda kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada ya kubainika kuwa inabana taarifa kwa umma.
Naibu Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Charles Stuart akimkabidhi tuzo ya Funguo la dhahabu Afisa Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima Ya Afya (NHIF), Shani Mussa walioibuka washindi wa kwanza upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakifuatilia mada kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA