ODINGA: NI SIKU YA KIHISTORIA KENYA NA KWA AFRIKA
Picha / Maktaba |
Mgombea urais wa upinzani Raila Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika.
Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais.
Imetoa mfano mwema.
"Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."
Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Naye Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka amesema mahakama imekuwa mfano mwema kwa Afrika na dunia nzima.
"Ninajivunia kuwa Mkenya leo," amesema.
"Sasa tutaangalia kina kuhusu tume ya uchaguzi. Hatuan imani kwamba wanaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki."
0 comments:
Post a Comment