Saturday, 2 June 2018

MAADHIMISHO WIKI YA MAZINGIRA YAWAKUTANISHA WADAU SEKTA YA UCHUKUZI

Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA Ally Changwila akifafanua mikakati inayofanywa na mamlaka hiyo kuhakikisha shughuli za anga zinakuwa rafiki kwa mazingira katika  maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam..


Wageni waliofika katika banda la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakitia saini katika kitabu cha wageni cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) katika maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam, (mwisho kulia) ni Afisa Habari wa TCAA Bestina Magutu


Wanafunzi waliofika katika banda la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA Ally Changwila  namna TCAA inavyothamini utunzaji wa mazingira nchini. 

Baadhi ya wafanyakazi wanaowakilisha mamlaka mbalimbali katika sekta ya uchukuzi wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano walipokuwa wakihudumia wananchi waliokuwa wakifika katika maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA