WANAMABADILIKO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA WILAYANI TARIME
"Shemeji zangu walikuwa sita walinipiga sana kwa kweli kwa sababu ya kutaka kumiliki Mali za Mume wangu ambaye ni Marehemu" , ni mmoja ya wanawake wa Tarime akisimlia kwa masikitiko kutokana na ukatili alioupata baada ya kufiwa na mumewe, ambapo ndugu wa mume alilazimisha kumrithi yeye na mali za mumewe. Mila kama hizi zinazomkandamiza mwanamke zinapaswa kusitishwa
"Tumekubali kabisa watoto wetu wa kike wasiendelee kukeketwa ,lakini bado jamii zetu hazituelewi tunaendelea kuwaelimisha ili nao wabadilike."- Mzee wa Kimila (Aliyesimama). Bado kuna kazi kubwa ya kumaliza swala la ukeketaji lakini kupitia elimu mbalimbali na mafunzo yanayotelewa kuhusu maswala ya ukeketaji juu ya hasara na madhara yake inaendelea kupunguza idadi ya wanaokeketwa.
"Kwa Tarime mwanamke kupigwa na kuvuliwa nguo hadhalani ilikuwa ni kitendo cha kawaida tu" - Sara Boniface (aliyesimama) , alielezea kwa kina kuhusu ukatili wa kupigwa ambapo aliongeza kwamba kwa sasa ukatili huo umepungua kutokana na elimu wanayoipata wanajamii juu ya ukatili wa kijinsia.
Mmoja wa wazee wa Kimira kutoka Tarime(aliyesimama) akieleza juu ya ukeketaji na kudai kuwa mwanamke aliyekeketwa anakuwa na thamani kubwa kama ilivyo kwa mwanamke mweupe kwa wasukuma, hii ni moja ya sababu zinazosababisha ukeketaji uendelee. Ikiwa elimu itaendelea kutolewa ukeketaji huu utapungua kwa kiasi kikubwa.
"Ukatili wa ukeketaji ulikuwa unafanyika hadharani kweupe, wazazi walikuwa wanalazimisha mabinti zao kukeketwa ili wapate mahali nyingi zaidi, ambapo fedha hizo ziwasaidie katika kupata kipato zaidi" - Nyakerandi Mariba. Swala hili limepungua sana kutokana na juhudi za wanamabadiliko kuendelea kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia.
"Maswala ya ukatili wa kijinsia yanaleta madhara makubwa katika jamii zetu,hasa kwa mabinti na akina mama"-Lucy Matemba Afisa maendeleo ya jamii Tarime
Meneja wa kampeni ya Tunaweza Bi. Eunice Mayengela akiendelea kutoa Muongozo wa majadiliano
Wanamabadiliko wakiendelea kufuatilia mjadala
"Kila wiki tunapokea kesi zaidi ya kumi (10) zanazoripotiwa Tarime zikihusu kipigo,ubakaji, ulawiti na wanawake kutishiwa kuuwa,kupigwa sana kisha kubakwa kwa lazima ama kulawitiwa"- Dawati la Jinsia . Licha ya kesi hizo kuwa nyingi lakini elimu inayoendelea kutolewa na kampeni ya tunaweza imesaidia sana kupunguza ukatili wa kijinsia.
Wazee wa Kimila kutoka Tarime wakiteta jambo wakati wa mjadala
Wanamabadiliko wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha na Fredy Njeje
0 comments:
Post a Comment