Friday 5 March 2021

REDIO VOICE OF AFRICA YAADHIMISHA MIAKA 10 KWA KUPANDA MITI HOSPITALI MPYA WILAYA YA MUHEZA


Mkurugenzi Mtendaji wa redio ya Voice of Africa (Aliyesimama) Bi.Chemuye Ngosha akimwagia maji mche wa mti kama ishara ya kuzindua zoezi la upandaji miti katika hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa


Wadau wa redio ya Voice of Africa wakishiriki katika kupanda miti katika hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa

Na Mwandishi Wetu

Katika kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwake redio ya Voice of Africa yenye masafa ya 98.5 yenye ofisi zake wilaya ya Korogwe mkoani Tanga iliratibu na kushiriki zoezi la upandaji miti 100  katika hospitali mpya ya wilaya ya muheza.

Akizungumzia uamuzi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa redio ya Voice of Africa Bi.Chemuye Ngosha amesema kwamba huo haukuwa uamuzi mgumu kuufanya kwani redio hiyo ni sehemu ya kuihudumia jamii na wakati huu ambapo imetimiza miaka kumi ulikuwa wakati muafaka wa kuweka alama katika jamii na hasa kwa kuyagusa mazingira kwa kupanda miti.

"Unaweza ukajiuliza kwanini miti hii 100 tumeamua kuipanda hapa hospitali,niseme tu kwamba licha ya kuwa itabaki kama alama ya kumbukumbu, mazingira na hali ya hewa hapa hospitali vitakuwa katika hali safi kabisa ya hewa na hivyo kufanyika chachu ya nafuu kwa wagonjwa na watu mbalimbali  watakaofika hapa kwa ajili ya kupata huduma" Alisema Bi.Chemuye

Mbali na zoezi la upandaji miti, miaka kumi ya Voice of Africa iliadhimishwa kwa tamasha lililofanyika katika viwanja vya CCM Jitegemee Muheza na kupambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo mazoezi,semina za kielimu kutoka taasisi mbalimbali zkiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Zimamoto, vipaji vya muziki pamoja na burudani za ngoma.

Akimwakilisha Mh.Mkuu wa Wilaya,Kaimu Mgeni Rasmi,Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Muheza  Bw.Shaban Selemani Maghembe amekipongeza kituo cha redio cha Voice of Africa kwa kufikia miaka kumi ya utendaji wenye kuyagusa moja kwa moja maisha ya wananchi na kutoa rai kuwa kazi hii iendelee na iboreshwe zaidi na zaidi kwani mafanikio hayatakiwi kuwa chanzo cha kubweteka bali yafanyike chachu ya kuwa bora zaidi.

Aidha katika hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji wa redio ya Voice of Africa ameishukuru Serikali kwa kuwapa vibali na ushauri na ushirikiano katika kipindi chote ambapo redio ipo hewani. Vilevile amewashukuru wadau wote wanaofanya kazi na redio hiyo zikiwemo kampuni na taasisi za ndani na nje ya nchi na kuahidi kuwa Voice of Africa itaendelea kuboresha huduma zake ili kuwafikia watu wengi zaidi hapa nchini.

Kituo cha redio cha Voice of Africa kilianzishwa  Februari 25,mwaka 2011 katika Wilaya ya Muheza na Decemba 2014 kituo hicho kilihamishiwa wilayani Korogwe. Voice of Africa inasikika mkoa mzima wa Tanga  kwa maana ya wilaya zote na katika mikoa jirani inasikika  Morogoro, Dodoma Manyara Kilimanjaro, Pwani na Visiwa vya Pemba,Unguja,Visiwa vya Comoro na Mafia.


Mkurugenzi Mtendaji wa redio ya Voice of Africa Bi.Chemuye Ngosha (kushoto) akimkaribisha jukwaani Kaimu Mgeni Rasmi,Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Muheza  Bw.Shaban Selemani Maghembe katika viwanja vya CCM Jitegemee Muheza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa 



Kaimu Mgeni Rasmi,Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Muheza  Bw.Shaban Selemani Maghembe akizungumza na wananchi waliojitokeza katika viwanja vya CCM Jitegemee Muheza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa 


Sehemu ya wananchi waliofika   katika viwanja vya CCM Jitegemee  Muheza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa


Bi.Beatrice Alfred kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) akitoa elimu kwa wananchi waliofika   katika viwanja vya CCM Jitegemee Muheza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa



Sharif salehe, Afisa Habari Jeshi la Zimamoto- Korogwe akitoa elimu kwa wananchi waliofika  katika viwanja vya CCM Jitegemee Muheza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka kumi ya redio ya  Voice of Africa


Burudani ya ngoma za asili


                                                                   Burudani ya mziki


0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA