VIKWAZO VYA UJASIRIAMALI KATIKA MFUMO WA DIJITI (DIGITAL)
Hizi ni kati ya sababu zinazofelisha wajasiriamali / wafanyabiashara wengi kuanzisha , kukuza na kufanikiwa katika biashara zao.
KASI YA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA
Tafiti zinaonyesha 93% za wafanyabiashara wadogo wadogo hutumia teknolojia na wanakiri inaendelea kukuza na kuwatangazia biashara.
Ili kuweza kutangaza biashara yako/bidhaa yako mitandaoni katika kipindi hiki cha techonolojia unatakiwa kuwa na kamera au simu yenye kamera nzuri. Picha nzuri ya bidhaa yako ndio kitu cha kwanza kwa mteja huvutiwa nacho na kuanza kufatilia bidhaa yako kupitia ukurasa wako. Lakini kutokana na gharama kubwa ya simu hizi zilizo na camera nzuri wafanyabiashara / wajasiliamali wachache wanaoweza kumudu kununua na kuitangaza /kukuza biashara zao.
GHARAMA ZA VIFURUSHI (DATA)
Bundle limekuwa kilio kwa vijana wengi hasa wanaofanya biashara mitandaoni, hasa biashara za hashtag, wanaotumia mitandao kufanya kazi za freelancing, wanaosoma kutipitia mitandaoni. Kama mfanyabishara unatakiwa kuwepo mtandaoni 24/7 ili kuweza kuopost, kuwasiliana na wateja. Lakini kutokana bei za bundle kuwa kubwa na vifurushi kupunguzwa vijana wengi wameshindwa kuwepo mtaondaoni 24/7.
Hasara yake ni kupoteza wateja, kupoteza ushawishi wa bidhaa yako mtandaoni. Muhimu serikali kuangalia hili ili kuweza kuwasaidia vijana kukuza biashara zao lakini pia nchi kukua katika sector ya digital, kumbuka data is life.
NDOA
Kati ya kikwazo kikubwa hasa kwa wanawake wanaojihusisha na biashara au ujasiliamali ni ndoa. Tafiti zinaonyesha wanawake wengi ambao hawapo kwenye ndoa ni wafanyabiashara kulinganisha na waliopo kwenye ndoa. Lakini pia tafiti zinaonyesha wanawake wengi wameacha kufanya biashara au ujasiliamali baada ya kuingia kwenye ndoa, kutokana na majukumu kuongezeka, hali za uzazi, lakini pia wanaume zao kuwakataza kufanya biashara sababu kubwa ni wivu wa kimapenzi.
Pia kuna baadhi ya ndoa wanaume hukataza wanawake kutumia simu, tukubaliane sote kuwa katika kipindi hiki cha technologia simu ni muhimu sana.
1. Kwa kutangaza bidhaa / biashara yako ili kuwafikia watu wengi
2. Kuongea na mteja hasa jinsi ya kufika dukani kwako au jinsi ya kupokea mzigo wake n.k
KUKOSA CHA KUFANYA
Vijana wengi hufanya biashara au kujiingiza katika ujasiliamali kutokana na kukosa cha kufanya hasa kipindi hiki ajira zilivyokuwa ngumu kupata. Ikitokea kijana kapata kazi (kuajiriwa) huacha kufanya biashara au kuendelea na ujasilimali. Lakini ni vyema tukakumbuka ni muhimu kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
JINSIA
Jamii za ki Africa zimetenganisha kazi kutokana na jinsia. Kazi ya mwanamke katika jamii nyingi ni mlezi, kufanya kazi zote za nyumbani wakati huo mwanaume akijulikana kama mtafutaji. Kupitia hii imefanya baadhi ya wanawake kutojiamini, kuwa na uoga na kushindwa kabisa kuanzisha biashara yoyote. Baadhi ya wanawake wameondoa hofu na wameweza kuanzisha biashara zao lakini kukosekana kwa mitaji mikubwa imepelekea kutokuza biashara zao.
Katika ulimwengu huu wa digitali wanawake wanatakiwa kufanya biashara zao ki digitali lakini kutokana na jamii nyingine kumkataza mwanamke kuwa na simu au kutumia simu imeafanya wanawake wengi kushindwa kuanzisha, kukuza, biashara zao hasa kupitia mitandao ya kijamii.
KUPANDA NA KUSHUKA KWA BIASHARA
Hakuna kitu kinapatikana kwa urahisi lakini pia hakuna maisha ya mtereko kuna milima na mabonde kwahiyo ukigundua hili ni rahisi kufanya biashara. Katika biashara kuna kipindi utauza sana na kupata pesa sana na ndio kipindi unatakiwa ujue jinsi ya kujitangaza, kutumia pesa na kukuza biashara yako, kuna kipindi biashara huwa ngumu sana na hapa wengi hukata tamaa na kuona bora waaache kufanya biashara lakini hiki ndio kipindi cha kujifunza na kuwa na uvumilivu. Sala ni muhimu sana katika biashara yoyote.
DINI / IMANI
Ukiachana na tamaduni za AfriKa kuwa kikwazo katika kuanzisha biashara mbalimbali hasa kwa wanawake wakiamini kwamba sio kazi zao. Lakini pia tumeona baadhi za dini kuzuia waamini wao kufanya biashara fulani mfano; biashara ya pombe, uuzaji wa sigara wakiziona kuwa ni dhambi.
Mfano mwingine kuna baadhi ya dini haziruhusu waamini wao kufanya ujasiliamali wa kufuga baadhi ya mifugo wakiamini ni haramu.
KUTOJUA NJIA ZA KUPATA MASOKO
Ni muhimu kwa mfanyabiashara kujua mbinu tofauti tofauti za kupata masoko, katika kipindi hiki cha dijiti watu wengi hujitangaza kupitia mitandao ya kijamii yaani facebook, twiiter, WhatsApp, na Instagram. Hii mitandao ya kijamii ina njia zake pia za kujitangaza ambazo zimetofautiana pia kama mfanyabiashara au mjasiliamali unatakiwa kuzijua, mfano; ku sponsor tangazo ( kwa Instagram), kutumia markert place ( kwa facebook), kupost status kwa uchache ( whatsApp). Hizi zote ni njia za kutafuta masoko kupitia mitandao.
Ni muhimu sana kwa mfanyabiashara au mjasiliamali kufanya ‘sale’( mnada) mara kadhaa sio kwa sababu bidhaa zimekuwa nyingi unataka utoe hapana. Faida ya kufanya sale ni kujenga uaminifu kwa wateja zako. Kupitia kufanya mnada wateja watapeana taarifa na hivyo kuongeza idadi ya wateja / watu wanaojua biashara yako. Hivyo kutojua njia za kupata masoko huzui biashara kukua na mwisho inakufa kabisa kutokana na ushindani kuwa kubwa sana.
0 comments:
Post a Comment