Showing posts with label DIJITI. Show all posts
Showing posts with label DIJITI. Show all posts

Thursday, 15 December 2022

VITU VYA KUEPUKA KATIKA MITANDAO UNAPOFANYA BIASHARA


Na Phenty Kiria

Mpendwa msomaji wangu, karibu katika mfululizo wa makala zetu. Leo nakuletea  elimu ya nini uepuke unapokuwa unafanya biashara yako mtandaoni. Bila ya shaka hakuna aliyeanzisha na anayefanya biashara anatamani apate faida na pia ikue. Baadhi ya wafanyabishara mitandaoni wamekuwa wakilalamika kuwa biashara zao hazikui japokuwa wana sponsor page zao, wanalipa waraghabishi kutangaza biashara zao. Zipo sababu nyingi lakini hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kutokukua na kudumaa kwa biashara mitandaoni tafadhali ziepuke;

 

  KUTOWEKA BEI YA BIDHAA

Wafanyabiashara wengi sasa hivi hawataki/ hawapendi kuweka bei ya bidhaa kwa sababu wanataka kuuza bei tofauti kutokana na mtu atakae mtafuta. Mfano mtu yeyote maarufu akimuulizia bei atamtajia bei kubwa akiamini ana pesa, au mtu ambae hamjui atamuuzia bei ya kawaida. Lakini pia watu wengi hawapendi kumfuata mtu DM wengine wanaona uvivu, wengine wanajua dalali au tapeli. Kuweka bei ya bidhaa inafaida nyingi

1. Kuongeza uaminifu kwa wateja

2. Kukuza biashara yako

3. Kuongeza wafuasi katika ukurasa wako wa biashara

 ( ambao ndio wateja wenyewe)

4. Husaidia katika utafutaji masoko ( marketing ); kuna muda utahitaji kufanya sales sasa ni muhimu mteja kujua bei imetoka wapi na imeshuka kwa kiasi gani

5. Kupunguza usumbufu wa kuulizwa bei kila mara.

 

KUFUNGA SEHEMU YA UJUMBE (DM)  

Mitandaoni kuna baadhi ya watu ni wasumbufu sana ndio maana watu wengi hawapendi kuacha sehemu zao za ujumbe wazi lakini wewe kama mfanyabiashara unaetaka kukuza biashara yako unahitaji kuacha sehemu yako ya ujumbe wazi ili mteja aweze kuwa uhuru kuuliza kitu chochote. Lakini wafanyabiahara wengi wamekuwa na tabia ya kufunga sehemu zao za ujumbe, wengi wakiandika kabisa “usije sehemu za ujumbe piga simu” hii ni mbaya kwa sababu unapoteza wateja wengi sana bila kujua, na sio kila mtu anapenda kuongea na simu.

Kama mfanyabiashra na hupendi shida zinazotokana na sehemu za ujumbe nakushauri mtafute mtu atakaekuwa ana manage ukurasa wako hata kama kwa kumlipa au kutomlipa ili aweze kujibu jumbe za watu lakini pia kujibu kwa wakati.

 


KUWEKA UKURASA WAKO PRIVATE

Wafanyabiashara wengi hawana elimu juu ya biashara za mtandaoni wengi wamenza biashara hii bila kujua nini wanatakiwa kufanya na nini hawatakiwi kufanya, watu wengi (Instagram na twitter) wameweka kurasa zao private lakini pia baadhi ya wafanyabiashara  wameweka kurasa zao private. 

Kuweka ukurasa wako private wewe kama mfanyabiashara inakupotezea fursa nyingi sana bila wewe kujua maana wateja wako watakuwa ni wale wale wa kila siku waliopo mpaka pale utakapoamua wewe kuongeza. Lakini pia kuna watu wengine watapenda kuongea na wewe jinsi ya kukusapoti na wakashindwa kutokana na kuwa private.

    



KUWEKA UJUMBE KUFUTIKA BAADA YA MUDA (DISAPPEARING MESSAGE)

Mtandao wa WhatsApp umeleta madaliko mtu anaweza kuweka jumbe zake kupotea kila baada muda fulani. Hii kwa mfanyabishara sio nzuri maana unapoteza taarifa muhimu za mteja wako, mfano mtu alikuuliza bei ya bidhaa zako lakini hakununua ila baada ya wiki akarudi nakusema anataka ile bidhaa, na ujumbe wake ushapote, hivyo itakupasa kuanza kuulizia upya ni nini anataka wateja wengine hawapendi na wanaweza wasijibu na hivyo wasinunue pia.

 

 

   EPUKA KUWEKA MAELEZO MAREFU / KUTOWEKA KABISA

(CAPTION)

Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanapenda kuandika vitu vingi sana wanapotangaza biashara zao lakini pia wapo wasioandika kabisa, wote hawa wanafanya vitu tofauti lakini wote wanapoteza wateja. Sio kila mtu anapenda kusoma hivvo akiona maneno mengi anapita tuu, huyu asie andika kabisa mtu hawezi elewa bei au anapatikana wapi nk. Andika kwa ufupi ili uweke urahisi wateja zako kusoma, mfano

         “Dawa ya kuzuia meno kuuma na kuoza

           Bei; ………..

           Piga/ WhatsApp: ……..”

Hakikisha tangazo lako linaelezea faida ya bidhaa yako yaani kwa nini mteja anunue bidhaa yako? Bila kuelezea faida ya bidhaa yako mteja hawezi jua kwa nini anunue kitu chako asinunue kwa mtu mwingine.

 

LUGHA

Ni vizuri ukajua soko lako ni lipi, ukishajua soko lako ni lipi unaweza jua ni lugha ipi utumie mara nyingi. Mfano ukijua soko lako lipo Uganda, Kenya na Zambia kuliko Tanzania basi ni vizuri ukatumia kingereza mara kwa mara lakini kama soko lako unaona lipo Tanzania ni vizuri Kiswahili mara nyingi ili kupata wateja sio kwamba usitumie kingereza kabisa, hapana

   Ki bongo bongo watu wakiona kingereza kingi katika matangazo yako wanajua bei ni kubwa hata hawaangalii tena bei wanapita tuu. Hivyo fanya tafiti  jua wateja wako wanaokuja mara kwa mara kununua au kuulizia bei wanatumia lugha gani, hii ni njia moja wapo ya kuweza kujua soko lako lipoje.

  

USIFUTE MAZUNGUMZO YAKO NA MTEJA.

Tunashauri kutofuta mazungumzo yako na mteja hata kama amenunua tayari bidhaa yako, kwa nini? Sio kila mtu atapenda kazi yako mtu anaweza sema amelipia bidhaa yako na hajapokea na uthibitisho wa kutuma pesa akatuma mtandoni hii moja kwa moja utaitwa tapeli na madhara yake ni makubwa maana utapoteza wateja wote hata wa zamani ambao walishanunua kwako. 

Lakini kama ama una mazungumzo yote mliofanya unaweza weka picha zake (screenshort) na kila mmoja akaona kwamba ni kweli alipokea mzigo wake, ni muhimu kumuuliza mteja kama kapokea mzigo wake, pia  kumwambia karibu tena sio akaribie tu tena siku nyingine lakini ni ishara kwamba mzigo umemfikia. Naomba kuwakumbusha kuwa  kujenga brand ni kazi ngumu sana lakini kuibomoa ni rahisi sana.

 

Vipo vitu vingi visohitajika katika biashara za mitandaoni lakini hizi za leo ni vitu vikubwa vya kutofanya. Teknolojia inakuja na faida zake lakini pia na changamoto zake ni vizuri tukatumia mitandao kama njia ya kutuongezea vipato au njia ya kukuza akili zetu.              


Ni Imani yangu kuwa mwaka 2023 utaenda kupiga hatua kubwa katika namna ya uendeshaji wa biashara yako mtandaoni..... NAKUTAKIA HERI YA MWAKA MPYA

Saturday, 3 December 2022

TUMIA MITANDAO HII KUTANGAZA NA KUKUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI






Na Phenty Kiria

Teknolojia imerahisisha mambo mengi ikiwemo biashara. Kupitia mitandao ya kijamii wengi wameweza kutangaza biashara au ujuzi na kupata matokeo chanya. Hii ni kutokana na urahisi wa kusambaza na kupeleka Taarifa pamoja na wepesi wa muingiliano katika mitandao hii.

Kwa kuanza ni vyema tukaifahamu baadhi ya mitandao ya kijamii yenye watumiaji wengi ambayo pia yaweza kutumika kama fursa ya kukuza na kuitangaza biashara yako.

I. Facebook (FB)

II. Instagram (IG)

III. WhatsApp

IV. Twitter

V. LinkedIn

VI. YouTube

VII. Reddit

VIII. Pinterest

IX. Tiktok

Lakini kupitia makala hii nitaelezea japo kwa ufupi mitandao inayofanya vizuri zaidi na kutumiwa na watu wengi katika biashara na mbinu za  kuitangaza biashara yako katika mitandao hiyo;

 

 


1. FACEBOOK

Facebook inawatumiaji zaidi ya 2.91 bilioni (active users) nakufanya kuwa mtandao bora na mkubwa katika biashara. Kwanza ni muhimu ukaweka ukurasa wako kuwa ukurasa wa biashara. Jinsi ya kutangaza na kukuza biashara yako kupitia facebook.

· Market place; hii ni sehemu unaweka biashara yako na kuwafikia watu wengi, kumbuka kuweka namba ya simu, na bei. Wafanyabiashara wengi hawapendi kuweka bei hii inawafanya wateja kukimbia. Lakini pia kwa watu wavivu hawawezi kukufuata kuanza kuulizia bei. Unashauriwa kuweka bei kwa kuepusha usumbufu lakini pia kutopoteza wateja.

 

· Tumia makundi; kwa sasa facebook imekuwa na kundi mengi sana ya biashara na inawafuasi zaidi 500 (followers). Mfano grop la madalali, group la wauza vitu vilivyotumika, group la chakula kizuri n.k, mengi unaposti bure na mengine unaposti kwa pesa. Tumia njia hii ili kuwafikia watu wengi zaidi.

 



 

2. INSTAGRAM

Ukitoka mtandao wa Facebook kuwa na watuamiaji wengi Instagram ndio mtandao unafuta kwa watumiaji. Kwa hii tafiti tu inaonyesha ni sehemu nzuri ya kutangaza na kukuza biashara yako. Zipo njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia kuitangaza biashara yako kupitia mtandao wa instagram; zifuatazo ni njia chache kati ya hizo

· Mraghabishi (Influencers); hawa ni watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii, watu wengi wanawafatilia lakini pia wanajulikana sana mitandaoni. Hivyo tengeneza  bajeti yako ya kutafuta masoko na ujue utahitaji walaghabishi wangapi. Faida ya hii unaweza usipate mteja kwa wakati huo huo lakini watu wakaijua biashara yako na wakihitaji kwa baadae, pia watu wakaanza kukufatilia ukurasa wako.

 

· Anzisha challenge; ukiwa tayari na wafuasi wa kutosha unaweza anzisha challenge. Mfano; piga picha na bidhaa yetu yoyote na tag ukurasa wetu atakaepata ‘like’ nyingi anapewa bidhaa zetu mbili bure. AU posti picha ya bidhaa zetu na utag ukurasa wetu na upate bidhaa yetu moja bure. Hii itakufanya ujuliakane lakini pia upate wateja wapya.

 

· Sponsor ADS; saivi unaweza kutagaza biashara yako kwa ku sponsor tangazo kwa gharama nafuu inaanzia siku moja mpaka miezi. Tunashauri uanze ku sponsor tangazo kuanzia siku mbili na kuendelea.

 

Kumbuka kuweka ukurasa wako kuwa ukurasa wa biashara ili ukusaidie kujua ni watu wangapi wameona tangazo lako, wangapi wametunza tangazo lako kwa matumizi ya baaadae n.k



3. WHATSAPP

Watu wengi wanasema WhatsApp sio mtandao wa kutangaza biashara lakini kuna vitu hawajui kuna umuhimu wa kujua njinsi ya kutumia whatsApp

· Hakikisha unalihifadhi  jina la mteja wako; ni muhimu kutunza jina la mteja wako lakini inakupasa kumwambia atunze pia namba yako ili aweze kuona picha za bidhaa yako haijalishi kanunua au hajanunua kitendo cha kukufata WhatsApp inamaanisha kaona tangazo lako mahali kavutiwa nalo na anataka kujua kitu fulani hivyo hata kama hata nunua hakikisha una save namba yake ili aweze kuona bidhaa zako nyingine.

 · Kuposti status; wafanyabiashara wanaamini kupost bidhaa zao nyingi ndio kupata wateja, ni muhimu kuelewa kwamba kuposti bidhaa nyingi status ni kupunguza umakini wa mteja, hakuna mtu anataangalia picha zote kama ni nyinyi. Unashauriwa kuposti picha 10 kwa siku na kwa muda tofauti tofauti.

 · Tengeneza makundi; ili kupata wateja wa kutosha ni muhimu kutengeza makundi ambayo kila mzigo mpya ukiingia unatuma katika hilo kundi. Ni rahisi sana muhimu ni kutengeza kiungo (link) na kuzimbaza mitandaoni ili kuwaruhusu wateja wajiunge wenyewe.

 

 


 

4. TWITTER

Huu mtandao wafanyabiashara wengi hawatumii kutangaza biashara zao, wengi wanaona kama mtandao wa wasomi na wajuaji. Lakini huu ni kati ya mitandao ambayo unaweza kukutangaza na kukuza biashara na pia watumiaji wake ni wateja ambao kwa kiwango kikubwa sio wasumbufu. Naomba uzingatie kuwa, ni muhimu kuwa makini na kuwa mwaminifu katika kufanya biashara mtandaoni.

 

· Mraghabishi (Influencers); twiiter pia kuna walaghabishi ambao unaweza kualipa na kukusaidia kutangaza biashara yako. Ni muhimu kujua bajeti yako, unaweza ukatumia waraghabishi wachache lakini wenye ushawishi mkubwa au ukatumia walaghabishi wengi wenye ushawishi wa kawaida na kuwafikia watu wengi, kuna utofauti hapo lakini kwanza jua bajeti yako kwanza.

 

Kwa uchache hii ni kati ya mitandao  ambayo unaweza kuanzisha na kukuza  biashara yake na kupata faida. Unachotakiwa kufanya ni posti biashara yako kila siku, hii inajenga uaminifu kwa mteja lakini inakuongezea wateja wapya. Jitahidi sana kuposti mirejesho ya wateja katika ukurasa wako, mfano “ nguo yako ni nzuri sana nimeipenda/ ameipenda, chakula ni kitamu sana” hii inasaidia sana kujenga uaminifu  kwa wateja wasio kujua lakini pia watu kutamani/ kujaribu kutumia huduma yako.

Naomba nikukumbushe kuwa  uaminifu ni kitu muhimu sana kwa biashara za mitandaoni kutokana na wafanyabishara wengi kuwa matapeli.

Monday, 21 November 2022

VIKWAZO VYA UJASIRIAMALI KATIKA MFUMO WA DIJITI (DIGITAL)

 

Na Phenty Kiria

Hizi ni kati ya sababu zinazofelisha wajasiriamali / wafanyabiashara wengi kuanzisha , kukuza na kufanikiwa katika biashara zao.

KASI YA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA

Tafiti zinaonyesha 93% za wafanyabiashara wadogo wadogo hutumia teknolojia na wanakiri inaendelea kukuza na kuwatangazia biashara.

Ili kuweza kutangaza biashara yako/bidhaa yako mitandaoni katika kipindi hiki cha techonolojia unatakiwa kuwa na kamera au simu yenye kamera nzuri. Picha nzuri ya bidhaa yako ndio kitu cha kwanza kwa mteja huvutiwa nacho na kuanza kufatilia bidhaa yako kupitia ukurasa wako. Lakini kutokana na gharama kubwa ya simu hizi zilizo na camera nzuri  wafanyabiashara / wajasiliamali wachache wanaoweza kumudu kununua na kuitangaza /kukuza biashara zao.  

 

 GHARAMA ZA VIFURUSHI (DATA)

Bundle limekuwa kilio kwa vijana wengi hasa wanaofanya biashara mitandaoni, hasa biashara za hashtag, wanaotumia mitandao kufanya kazi za freelancing, wanaosoma kutipitia mitandaoni. Kama mfanyabishara unatakiwa kuwepo mtandaoni 24/7 ili kuweza kuopost, kuwasiliana na wateja. Lakini kutokana bei za bundle kuwa kubwa na vifurushi kupunguzwa vijana wengi wameshindwa kuwepo mtaondaoni 24/7.

Hasara yake  ni kupoteza wateja, kupoteza ushawishi wa bidhaa yako mtandaoni. Muhimu serikali kuangalia hili ili kuweza kuwasaidia vijana kukuza biashara zao lakini pia nchi kukua katika sector ya digital, kumbuka data is life.

NDOA 

Kati ya kikwazo kikubwa hasa kwa wanawake wanaojihusisha na biashara au ujasiliamali ni ndoa. Tafiti zinaonyesha  wanawake wengi ambao hawapo kwenye ndoa ni wafanyabiashara kulinganisha na waliopo kwenye ndoa. Lakini pia tafiti zinaonyesha wanawake wengi wameacha kufanya biashara au ujasiliamali baada ya kuingia kwenye ndoa, kutokana na majukumu kuongezeka, hali za uzazi, lakini pia wanaume zao kuwakataza kufanya biashara sababu kubwa ni wivu wa kimapenzi.

 

Pia kuna baadhi ya ndoa wanaume hukataza wanawake kutumia simu, tukubaliane sote kuwa katika kipindi hiki cha technologia simu ni muhimu sana.

1. Kwa kutangaza bidhaa / biashara yako ili kuwafikia watu wengi

2.  Kuongea na mteja hasa jinsi ya kufika dukani kwako au jinsi ya kupokea mzigo wake n.k

 KUKOSA CHA KUFANYA

Vijana wengi hufanya biashara au kujiingiza katika ujasiliamali kutokana na kukosa cha kufanya hasa kipindi hiki ajira zilivyokuwa ngumu kupata. Ikitokea kijana kapata kazi  (kuajiriwa) huacha kufanya biashara au kuendelea na ujasilimali. Lakini ni vyema tukakumbuka ni muhimu kuwa na vyanzo vingi vya mapato.

 


JINSIA

Jamii za ki Africa zimetenganisha kazi kutokana na jinsia. Kazi ya mwanamke katika jamii nyingi ni mlezi, kufanya kazi zote za nyumbani wakati huo mwanaume akijulikana kama mtafutaji. Kupitia hii imefanya baadhi ya wanawake kutojiamini, kuwa na uoga na kushindwa kabisa kuanzisha biashara yoyote. Baadhi ya wanawake wameondoa hofu na wameweza kuanzisha biashara zao lakini kukosekana kwa mitaji mikubwa imepelekea kutokuza biashara zao.

Katika ulimwengu huu wa digitali wanawake wanatakiwa kufanya biashara zao ki digitali lakini kutokana na jamii nyingine kumkataza mwanamke kuwa na simu au kutumia simu imeafanya wanawake wengi kushindwa kuanzisha, kukuza, biashara zao hasa kupitia mitandao ya kijamii.

 

KUPANDA NA KUSHUKA KWA BIASHARA

Hakuna kitu kinapatikana kwa urahisi lakini pia hakuna maisha ya mtereko kuna milima na mabonde kwahiyo ukigundua hili ni rahisi kufanya biashara. Katika biashara kuna kipindi utauza sana na kupata pesa sana na ndio kipindi unatakiwa ujue jinsi ya kujitangaza, kutumia pesa na kukuza biashara yako,  kuna kipindi biashara huwa ngumu sana na hapa wengi hukata tamaa na kuona bora waaache kufanya biashara lakini hiki ndio kipindi cha kujifunza na kuwa na uvumilivu. Sala ni muhimu sana katika biashara yoyote. 

DINI / IMANI

Ukiachana na tamaduni za AfriKa kuwa kikwazo katika kuanzisha biashara mbalimbali hasa kwa  wanawake wakiamini kwamba sio kazi zao. Lakini pia tumeona baadhi za dini kuzuia waamini wao kufanya biashara fulani mfano; biashara ya pombe, uuzaji wa sigara wakiziona kuwa ni dhambi. 

Mfano mwingine kuna baadhi ya dini haziruhusu waamini wao kufanya ujasiliamali wa kufuga baadhi ya mifugo wakiamini ni haramu.

 

 KUTOJUA NJIA ZA KUPATA MASOKO

Ni muhimu kwa mfanyabiashara kujua mbinu tofauti tofauti za kupata masoko, katika kipindi hiki cha dijiti watu wengi hujitangaza kupitia mitandao ya kijamii yaani facebook, twiiter, WhatsApp, na Instagram. Hii mitandao ya kijamii ina njia zake pia za kujitangaza ambazo zimetofautiana pia kama mfanyabiashara au mjasiliamali unatakiwa kuzijua, mfano; ku sponsor tangazo ( kwa Instagram), kutumia markert place ( kwa facebook), kupost status kwa uchache ( whatsApp). Hizi zote ni njia za kutafuta masoko kupitia mitandao.

Ni muhimu sana kwa mfanyabiashara au mjasiliamali kufanya ‘sale’( mnada) mara kadhaa sio kwa sababu bidhaa zimekuwa nyingi unataka utoe hapana. Faida ya kufanya sale ni kujenga uaminifu kwa wateja zako. Kupitia kufanya mnada wateja watapeana taarifa na hivyo kuongeza idadi ya wateja / watu wanaojua biashara yako. Hivyo kutojua njia za kupata masoko huzui biashara kukua na mwisho inakufa kabisa kutokana na ushindani kuwa kubwa sana.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA