Saturday, 3 December 2022

TUMIA MITANDAO HII KUTANGAZA NA KUKUZA BIASHARA YAKO MTANDAONI






Na Phenty Kiria

Teknolojia imerahisisha mambo mengi ikiwemo biashara. Kupitia mitandao ya kijamii wengi wameweza kutangaza biashara au ujuzi na kupata matokeo chanya. Hii ni kutokana na urahisi wa kusambaza na kupeleka Taarifa pamoja na wepesi wa muingiliano katika mitandao hii.

Kwa kuanza ni vyema tukaifahamu baadhi ya mitandao ya kijamii yenye watumiaji wengi ambayo pia yaweza kutumika kama fursa ya kukuza na kuitangaza biashara yako.

I. Facebook (FB)

II. Instagram (IG)

III. WhatsApp

IV. Twitter

V. LinkedIn

VI. YouTube

VII. Reddit

VIII. Pinterest

IX. Tiktok

Lakini kupitia makala hii nitaelezea japo kwa ufupi mitandao inayofanya vizuri zaidi na kutumiwa na watu wengi katika biashara na mbinu za  kuitangaza biashara yako katika mitandao hiyo;

 

 


1. FACEBOOK

Facebook inawatumiaji zaidi ya 2.91 bilioni (active users) nakufanya kuwa mtandao bora na mkubwa katika biashara. Kwanza ni muhimu ukaweka ukurasa wako kuwa ukurasa wa biashara. Jinsi ya kutangaza na kukuza biashara yako kupitia facebook.

· Market place; hii ni sehemu unaweka biashara yako na kuwafikia watu wengi, kumbuka kuweka namba ya simu, na bei. Wafanyabiashara wengi hawapendi kuweka bei hii inawafanya wateja kukimbia. Lakini pia kwa watu wavivu hawawezi kukufuata kuanza kuulizia bei. Unashauriwa kuweka bei kwa kuepusha usumbufu lakini pia kutopoteza wateja.

 

· Tumia makundi; kwa sasa facebook imekuwa na kundi mengi sana ya biashara na inawafuasi zaidi 500 (followers). Mfano grop la madalali, group la wauza vitu vilivyotumika, group la chakula kizuri n.k, mengi unaposti bure na mengine unaposti kwa pesa. Tumia njia hii ili kuwafikia watu wengi zaidi.

 



 

2. INSTAGRAM

Ukitoka mtandao wa Facebook kuwa na watuamiaji wengi Instagram ndio mtandao unafuta kwa watumiaji. Kwa hii tafiti tu inaonyesha ni sehemu nzuri ya kutangaza na kukuza biashara yako. Zipo njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia kuitangaza biashara yako kupitia mtandao wa instagram; zifuatazo ni njia chache kati ya hizo

· Mraghabishi (Influencers); hawa ni watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii, watu wengi wanawafatilia lakini pia wanajulikana sana mitandaoni. Hivyo tengeneza  bajeti yako ya kutafuta masoko na ujue utahitaji walaghabishi wangapi. Faida ya hii unaweza usipate mteja kwa wakati huo huo lakini watu wakaijua biashara yako na wakihitaji kwa baadae, pia watu wakaanza kukufatilia ukurasa wako.

 

· Anzisha challenge; ukiwa tayari na wafuasi wa kutosha unaweza anzisha challenge. Mfano; piga picha na bidhaa yetu yoyote na tag ukurasa wetu atakaepata ‘like’ nyingi anapewa bidhaa zetu mbili bure. AU posti picha ya bidhaa zetu na utag ukurasa wetu na upate bidhaa yetu moja bure. Hii itakufanya ujuliakane lakini pia upate wateja wapya.

 

· Sponsor ADS; saivi unaweza kutagaza biashara yako kwa ku sponsor tangazo kwa gharama nafuu inaanzia siku moja mpaka miezi. Tunashauri uanze ku sponsor tangazo kuanzia siku mbili na kuendelea.

 

Kumbuka kuweka ukurasa wako kuwa ukurasa wa biashara ili ukusaidie kujua ni watu wangapi wameona tangazo lako, wangapi wametunza tangazo lako kwa matumizi ya baaadae n.k



3. WHATSAPP

Watu wengi wanasema WhatsApp sio mtandao wa kutangaza biashara lakini kuna vitu hawajui kuna umuhimu wa kujua njinsi ya kutumia whatsApp

· Hakikisha unalihifadhi  jina la mteja wako; ni muhimu kutunza jina la mteja wako lakini inakupasa kumwambia atunze pia namba yako ili aweze kuona picha za bidhaa yako haijalishi kanunua au hajanunua kitendo cha kukufata WhatsApp inamaanisha kaona tangazo lako mahali kavutiwa nalo na anataka kujua kitu fulani hivyo hata kama hata nunua hakikisha una save namba yake ili aweze kuona bidhaa zako nyingine.

 · Kuposti status; wafanyabiashara wanaamini kupost bidhaa zao nyingi ndio kupata wateja, ni muhimu kuelewa kwamba kuposti bidhaa nyingi status ni kupunguza umakini wa mteja, hakuna mtu anataangalia picha zote kama ni nyinyi. Unashauriwa kuposti picha 10 kwa siku na kwa muda tofauti tofauti.

 · Tengeneza makundi; ili kupata wateja wa kutosha ni muhimu kutengeza makundi ambayo kila mzigo mpya ukiingia unatuma katika hilo kundi. Ni rahisi sana muhimu ni kutengeza kiungo (link) na kuzimbaza mitandaoni ili kuwaruhusu wateja wajiunge wenyewe.

 

 


 

4. TWITTER

Huu mtandao wafanyabiashara wengi hawatumii kutangaza biashara zao, wengi wanaona kama mtandao wa wasomi na wajuaji. Lakini huu ni kati ya mitandao ambayo unaweza kukutangaza na kukuza biashara na pia watumiaji wake ni wateja ambao kwa kiwango kikubwa sio wasumbufu. Naomba uzingatie kuwa, ni muhimu kuwa makini na kuwa mwaminifu katika kufanya biashara mtandaoni.

 

· Mraghabishi (Influencers); twiiter pia kuna walaghabishi ambao unaweza kualipa na kukusaidia kutangaza biashara yako. Ni muhimu kujua bajeti yako, unaweza ukatumia waraghabishi wachache lakini wenye ushawishi mkubwa au ukatumia walaghabishi wengi wenye ushawishi wa kawaida na kuwafikia watu wengi, kuna utofauti hapo lakini kwanza jua bajeti yako kwanza.

 

Kwa uchache hii ni kati ya mitandao  ambayo unaweza kuanzisha na kukuza  biashara yake na kupata faida. Unachotakiwa kufanya ni posti biashara yako kila siku, hii inajenga uaminifu kwa mteja lakini inakuongezea wateja wapya. Jitahidi sana kuposti mirejesho ya wateja katika ukurasa wako, mfano “ nguo yako ni nzuri sana nimeipenda/ ameipenda, chakula ni kitamu sana” hii inasaidia sana kujenga uaminifu  kwa wateja wasio kujua lakini pia watu kutamani/ kujaribu kutumia huduma yako.

Naomba nikukumbushe kuwa  uaminifu ni kitu muhimu sana kwa biashara za mitandaoni kutokana na wafanyabishara wengi kuwa matapeli.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA