TCAA ENDELEENI KUCHAPA KAZI KWA USHIRIKIANO
Watumishi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuendelea kutenda kazi kwa ufanisi.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi Mrope amewataka wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika Aprili 28,2023 mjini Morogoro.
"Tunatambua umuhimu wa TCAA katika maendeleo ya nchi yetu lakini TCAA inajengwa kuianzia na wewe mtumishi mmoja, nawasihi sana mfanye kazi kwa kushirikiana kila mmoja kwa nafasi yake na inapobidi msaidie mwingine ili kuhakikisha malengo ya taasisi na serikali kwa ujumla yanafikiwa na huduma inatolewa" amesema Bw.Mrope
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza S. Johari amesema Mamlaka inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo wa kuboresha Mfumo wa Masafa ya Mawasiliano wa Sauti baina ya rubani na waongozaji ndege katika vituo vyote vya kuongozea ndege nchini.
Baraza hilo limefanyika kwa siku moja ambapo mbali na kujadili masuala kadhaa yanayoihusu TCAA wajumbe wamepata nafasi ya kupiga kura na kumchagua mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka huu wa fedha.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Xavier Daudi Mrope akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la TCAA lililofanyika Aprili 28,2023 mjini Morogoro.
0 comments:
Post a Comment