MACHINGA ZAIDI YA 50 WAKUTANA KUJADILI SERA YA VIJANA TEMEKE
Kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Mulika Tanzania inatekeleza mradi wa Imarika ambao miongoni mwa mambo yanayotekelezwa ni kutoa elimu ya afya ya uzazi, stadi za maisha elimu, na ushiriki wa vijana katika maeneo ya uongozi yaliyolengwa mahususi kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa mitaani, wanaojulikana kwa jina la "Machinga," katika Wilaya ya Temeke Dar-es-Salaam.
Machinga zaidi ya 70 , wameshiriki warsha hii ambayo ni Utekelezaji wa awamu ya 2 ya Afua ya Imarika kwa lengo la kuipitia na kujadili sera ya maendeleo ya vijana (2007) inayotumika sasa na wajibu wa machinga katika sera hiyo lakini pia uainishaji wa vituo vya Afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mulika Tanzania Bw. Hussein Melele amesisitiza kuwa Mulika inawalenga zaidi vijana kwasababu ni kundi la upekee sana katika kuleta ustawi kwenye jamii kama litapatiwa taarifa, elimu na fursa sahihi.
"Kama ambavyo jina letu linasadifu, Lengo letu ni kuzimulika fursa kwenu ninyi vijana wenzetu ili kesho yetu ikawe bora zaidi ya leo. Nafahamu nyote ni wafanyabiashara ndogo ndogo pamoja na elimu ya afya ya uzazi, namna ya kupata mikopo isiyoumiza, kukutana kwenu ni eneo muhimu la kuwakutanisha ili mfahamiane na mbadilishane uzoefu, mnafahamu mahusiano chanya ndio mtaji mkuu katika kukua naomba sana mfahamiane na mjenge undugu utakaowafaa nyote" alisema Bw. Melele.
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Masalida Njashi aliwashukuru vijana kwa kutii wito na kuhudhuria warsha hiyo na kuwasihi wazingatie yote yatakayojadiliwa na kuwasisitiza kuutumia muda wao kusikiliza na kuuliza maswali ili kuhakikisha suala la sera ya Vijana.
Wakati wa kutoa elimu kuhusu sera ya vijana ya mwaka 2017, Afisa Maendeleo ya Vijana Kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Amina Sanga alijikita katika kueleza mchakato wa mwanzo wakati wa utengenezwaji wa sera hiyo mwaka 2017 ambapo amesisitiza yale yaliyokuwa yakitizamwa kama mambo mazito yamebadilika na sasa sera hii pamoja na yote inahitaji maboresho.
"Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 ilikuwa na changamoto ya utekelezaji kutokana na Mabadiliko tofauti tofauti. Sera mpya ya Maendeleo ya Vijana ijayo itakuwa na marekebisho ya namna ya utekelezaji wake ila nataka mfahamu kama vijana wenzangu, pamoja na yote sera hii imelenga katika kumjengea kijana wa Kitanzania ustawi bora kabisa katika nyanja za afya na uchumi. Serikali yetu pendwa imejipanga kuhakikish mazingira ya vijana ni bora sana kwa maslahi mapana ya taifa letu" alisisitiza Bi. Amina
Pia Bi. Amina amsesema Maboresho ya Sera ya Maendeleo vijana ya 2019, imeongeza maeneo mengine kulingana na mabadiliko ya kijamii na teknolojia. Maeneo hayo ni Afya ya Akili, Matumizi ya TEHAMA na Afya Ya Uzazi.
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, mfanyabiashara wa mashuka Katika soko la kariakoo Bw. Hamad Saidi ameishukuru Mulika Tanzania kwa kuandaa warsha hii kwani imeendelea kuwajengea uelewa mkubwa juu ya sera na mikakati ambayo ipo kwa ajili ya vijana.
Wakati wa awamu ya awali ya afua hii, Mulika Tanzania ilijikita katika kuwapa wachuuzi wa mitaani maarifa muhimu juu ya Uzazi wa Ngono Afya, ikiwa ni pamoja na mada kama vile ukatili wa kijinsia (GBV), stadi za maisha, ujuzi wa kifedha, na ujuzi wa uongozi.
Wakati programu ikiendelea katika awamu ya pili, wachuuzi wa mitaani walipewa taarifa za kina na mwongozo wa kupata mikopo kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA) na katika kuweka muendelezo wa elimu hii, Kati ya wachuuzi 70 wa mitaani, 10 walichaguliwa na kuwezeshwa na maarifa muhimu ili kuwa Wakufunzi wa Wakufunzi (ToT) kwa lengo kuwawezesha kuongoza na kusaidia wengine kwa ufanisi katika shughuli zao za kila siku.
0 comments:
Post a Comment