Showing posts with label tigo. Show all posts
Showing posts with label tigo. Show all posts

Tuesday, 31 October 2017

TIGO WAZINDUA KAMPENI MPYA YA TUMEKUSOMA





Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma wa kampuni ya Tigo, David Umoh, pamoja na Mtaalam wa Huduma kwa Wateja, Kitengo cha Biashara, Sarah Cyprian wakizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni mpya ya Tumekusoma inayoendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma *147*00#.  Namba *147*00#  itawawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi, pamoja na kupata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hiyo mpya.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandhishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa Kampeni mpya ya 'TUMEKUSOMA' inayokwenda sambamba na uzinduzi wa namba mpya ya huduma za Tigo (*147*00#) itakayowawezesha wateja wake kupata huduma mbalimbali kwa urahisi zaidi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kampuni hiyo, Makumbusho jijini Dar es sa salaam.


Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo imezindua rasmi kampeni mpya ya Tumekusoma, ambayo ni mkakati mkubwa wa kufikia wateja wake na bidhaa na huduma bora zinazoendana na mahitaji yao kwa muda muafaka. Kampeni hii ya Tumekusoma pia inaendana na uzinduzi wa namba mpya ya huduma ya *147*00# itakayowawezesha wateja wa Tigo kupata huduma mbali mbali za sauti na VAS kutoka Tigo kwa hatua rahisi zaidi. Wateja wa Tigo watakaotumia namba hiyo mpya pia watapata bonasi kubwa ya vifurushi na muda wa maongezi kila watakapotumia namba hii mpya.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ya Tumekusoma jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bidhaa na Huduma za Tigo, David Umoh alisema, ‘Tumesoma hitaji la watumiaji wa mitandao ya simu la menu au namba ya huduma ambayo itarahihisha hatua za kununua vifurushi au kufanya miamala ya fedha. Menu hii mpya inajibu mahitaji hayo yote. Ni rahisi sana kutumia. Pamoja na haya, namba mpya ya *147*00# inawapa wateja ofa kabambe ya nyongeza ya muda wa maongezi, SMS na data kila mara watakaponunua vifurushi kupitia namba hii,’ Umoh alisema.

Alibainisha faida nyingine kubwa ya menu hiyo mpya ni ofa za Chapchap, zinazowawezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vinavyoendana na mahitaji na tabia zao za kipekee za matumizi ya simu, jambo ambalo linaendana na lengo la Tigo la kuwaongezea thamani wateja wake. ‘Tumesoma mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho muafaka linaloendana na mahitaji yao ya kipekee kupitia menu hii inayorahisisha matumizi yao ya simu kupitia mtandao wetu ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini,’ alisema.

Tigo inaendelea kuwa mtandao unaoongoza kwa kuzindua bidhaa na huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja. Tigo ndio mtandao ulioleta mageuzi makubwa zaidi katika mifumo ya bei ya mitandao ya simu za mkononi nchini. 

Tigo pia ndio iliyokuwa mtandao wa kwanza kuzindua huduma za vifurushi vya sauti na data, ndio mtandao wa kwanza kuzindua simu za kisasa zenye mfumo wa lugha ya Kiswahili na pia ndio mtandao wa kwanza nchini kuzindua huduma ya Tigo Pesa iliyowezesha wateja wake kufanya miamala ya fedha nje ya nchi iliyokuwa na uwezo wa kubadili thamani ya fedha kulingana na thamani ya fedha ya nchi husika.

‘Kupitia Tumekusoma, tunawakaribisha wateja wote wa Tigo wajiunge nasi katika safari hii ya kumbukumbu ya hatua tulizopiga na mafanikio makubwa tuliyopata katika kipindi hiki cha kuwahudumia Watanzania. Tunawakaribisha nyote kuungana nasi katika mageuzi ya kidigitali nchini na kufurahia mtandao wetu wa Tigo ulioboreshwa na uliosambaa kote nchini Tanzania,’ Umoh alisema. 

Menu mpya iliyoboreshwa ya *147*00# inaanza kufanya kazi leo na wateja wa Tigo wanaweza kuanza kupata bonasi murwa kwa manunuzi yote wanayoyafanya. Tunawakaribisha wateja wetu wakae mkao wa kupokea ofa zaidi kabambe huku tukiendelea katika safari hii ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi zaidi na kwa ubora wa hali ya juu.

Friday, 11 August 2017

KILELE CHA NANE NANE BANDA LA TIGO -NGONGO LINDI

Baadhi ya wananchii wakiwa wamezunguka Banda la Tigo wakipata Huduma Mbalimbalia katika maonesho ya kilimo ya Nane nane yaliyopo Ngongo Mkoa wa Lindi.

Meneja wa kanda ya Kusini wa Kampuni ya Tigo  Uthman Madata akigawa Kofia Katika Banda la Tigo katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo ya Ngongo Mkoani Lindi

Meneja wa kanda ya Kusini wa kampuni ya mtandao wa  Tigo Uthman Madata akimuonesha Simu ya Mkononi Aina ya Tekno S1 Mwanafunzi wa Sekondari ya Lindi Charles Shirima katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane  yaliyofanyika Mkoani Lindi.

Meneja wa kanda ya Kusini kampuni ya mtandao wa Tigo akiongea na baadhi ya wateja wa Tigo waliofika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya Nanenane

Meneja wa kanda ya Kusini kampuni ya mtandao wa Tigo akiongea na baadhi ya wateja wa Tigo waliofika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya Nanenane​


Saturday, 19 December 2015

TIGO YADHAMINI UZINDUZI WA ROCK CITY MALL: KUFANYA GULIO LA KUUZA BIDHAA MBALIMBALI MWANZA

Meneja huduma kwa Wateja wa Tigo kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo(katikati),akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Mwanza jana,ambapo jengo la kimataifa la biashara(Rock City Mall) limekamilika na Tigo watafanya gulio la kuuza bidhaa mbalimbali,kushoto ni Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa Mwanza City Commercial Complex Company Limited Joseph Mlinzi na kulia ni Meneja wa Tigo pesa kanda ya Ziwa Issa Orry.
Meneja wa Tigo pesa kanda ya Ziwa Issa Orry,akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana,ndani ya jengo la kimataifa la biashara (Rock City Mall) ambapo limekamilika na Tigo  watafanya gulio la kuuza bidhaa mbalimbali,kushoto  ni Meneja huduma kwa Wateja wa Tigo kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo
Katibu wa Bodi ya wakurugenzi wa Mwanza City Commercial Complex Company Limited Joseph Mlinzi,akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza jana,kuhusu kukamilika kwa jengo la kimataifa la biashara(Rock City Mall),ambalo wananchiwanaruhusiwa kuingia na kununua bidhaa kuanzia jumamosi wiki hii,kulia ni Meneja huduma kwa Wateja wa Tigo kanda ya Ziwa Beatrice Kinabo,ambapo Tigo wataendesha gulio la kuuza bidhaa zao.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA