Showing posts with label zanzibar. Show all posts
Showing posts with label zanzibar. Show all posts

Friday, 6 January 2023

WAKUU WA TAASISI ZA SMT NA SMZ WAKUTANA ZANZIBAR


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Rashid A. Salim akizungumza na wakuu wa taasisi za SMT na SMZ katika mkutano wa wakuu wa taasisi kwenye tamasha la 9 la biashara Zanzibar.




Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latiffa Khamis akizungumza na wakuu wa taasisi za SMT na Serilikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika mkutano wa wakuu wa taasisi kwenye tamasha la 9 la biashara Zanzibar.

Wakuu wa Taasisi za Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo tarehe 6 Januari, 2023 wamekutana kwenye Tamasha la 9 la Biashara Zanzibar na kufanyanya mazungumzo yaliolenga kuendeleza ushirikiano katika kutatua changamoto na kuboresha huduma kwa Wafanyabiashara wa pande zote mbili.

Akizungumza katika Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Rashid A. Salim amesema kunachangamoto ambazo zinaweza kutatuliwa endapo Taasisi hizo zitashirikiana katika kupeana taarifa , kufanya mafunzo ya pamoja, kushiriki mikutano na kushirikiana katika kuaandaa miradi.

Ndugu Salim ameongeza  kuwa Mkutano huo ni hatua muhimu katika kudumisha Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana katika kuhahikisha Taasisi hizo zinawawezesha Wafanyabiashara Nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis amesema Mkutano huo umewaleta pamoja Wakuu wa Taasisi na kujadiliana mada zilizolenga kutatua changamoto katika usajili wa Biashara na leseni, Ushindani na halali, Viwango na Vipimo, Viwanda na Biashara.





Tuesday, 22 August 2017

MWAKILISHI WA JIMBO LA TUNGUU ASHIRIKI UJENZI WA SKULI YA MSINGI UZI NGAMBWA

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa na Wananchi wa jimbo lake katika kisiwa cha uzi ngambwa wakishangilia wakati wa ujenzi wa Taifa wa kujenga madarasa saba ya Skuli ya Msingi katika Kijiji cha Ngambwa kutowa elimu kwa watoto wa kijiji hicho kupata elimu ya msingi karibu na makaazi yao. Madarasa hayo yanajengwa kwa nguvu za Mwakilishi na Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo lao.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Kisiwa cha Uzi Ngambwa wakati wa ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi na nguvu Wananchi wa kijiji hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwahutubia wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambwa jimbo lake wakati wa ujenzi wa Taifa wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhani Abdallah akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Uzi Ngambw wakati wa ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Ngambwa. inayojengwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo la Tunguu na Nguvu za Wananchi wa Kijiji hicho.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akishiriki katika ujenzi wa skuli ya msingi uzi ngambwa.
Wananchi wa Ngambwa wakiwa katika ujenzi wa Skuli yao ya Msingi.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akishiriki katika ujenzi huo wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi.
Mwananchi wakishiriki katika ujenzi huo wa skuli ya msingi katika kisiwa cha Uzi kijiji cha Ngambwa.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa wakifuatilia hafla hiyo ya ujenzi wa Skuli yao mpya ya msinga katika kijiji chao.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohamed Said akiwa na bero likiwa na mchanga akishiriki katika ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa katika kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Jengo la madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa likiendelea na ujenzi wake.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa Uzi wakishiriki katika ujenzi wa madarasa katika kijiji hicho.
Wananchi wa kijiji cha Ngambwa kisiwa cha Uzi wakiwa katika ujenzi wa madarasa ya Skuli ya Msingi Ngambwa inayojengwa kwa nguvu na Mbunge na Mwakilishi kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu ZanzibarMhe. Simai Mohamed Said akizungumza na Mwananchi wa jimbo lake mkaazi wa Ngabwa Uzi Bi. Mwanaacha Khatib mkulima wa mwani wakati wa hafla ya ujenzi taifa wa skuli ya msingi ngambwa kisiwani humo.

Imetayarishwa na OthmanMapara Wa Zanzinews.com

Friday, 2 June 2017

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AKUTANA NA BALOZI WA MOROCCO


unnamed
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi wa Morocco katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Abdelilah Benryane wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo [Picha na Ikulu.] 02/06/2017.

Monday, 15 May 2017

BALOZI SEIF AFUNGUA TAMASHA LA TANO LA ZAHILFE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifungua Tamasha la Tano la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHILFE} kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani Zanzibar Riziki Pemba Juma kulia akiteta na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Mashindano ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} hapo katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amani Zanzibar Riziki Pemba Juma akitoa salamu za Wizara kwenye Tamasha la Mashindano ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} hapo katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Michezo na Serikali walioshuhudia ufunguzi wa Tamasha la Mashindano ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} hapo katika uwanja wa Amani.
Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar {BTMZ}, Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Ayoub Mohamed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas.
Balozi Seif akisalimiana na wachezi wa Timu ya Soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere { MNMA} waliopambana na Mabingwa watetezi wa Kombe la ZAHILFE Timu ya ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu { ZU}

Mabingwa watetezi wa Kombe la ZAHILFE Timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu { ZU} wakisalimiana na Balozi Seif ambae ni mgeni rasmi kwenye pambano lao dhidi ya Timu ya Soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere { MNMA} 
 Mashabiki wa Timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu { ZU} wakishangiria kwa kujiamini wakati Timu yao ilipotoa kichapo cha Paka mwizi cha Goli 4 kwa Bila dhidi ya Timu ya Soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Picha na – OMPR – ZNZ.

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu Zanzibar { ZAHILFE} Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu {Zanzibar University - ZU} jana ilidhihirisha ubabe wake baada ya kuitandika bila ya huruma Timu ya soka ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere { MNMA} Magoli 4-0.

Mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 ulifungua pazia la mashindao ya Tamasha la Michezo la Shirikisho hilo uliorindima ndani ya Uwanja wa Michezo wa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Watetezi hao ZU walionyesha dalili za mapema za ushindi wa mchezo huo licha ya kuwa mpaka wanakwenda mapumziko hakukuwa na timu iliyoona mlango wa mwezake huku washabiki wa Timu zote mbili wakishindwa kukaa kwenye majukwa ya uwanja huo.

Kipindi cha pili kilianza kwa mikiki mikiki kwa timu zote mbili lakini uzoefu na utaalamu wa Timu ya ZU ukajidhihirisha pale wanandinga hao walipoanza kumimina karamu ya Magoli ndani ya kimia cha MNMA na hadi mwisho wa mchezo huo ZU 4 na MNMA 0.

Akiizindua michezo hiyo ya Tamasha la Tano la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} tokea kuanzishwa kwake Mwaka 2013 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema utunzwaji wa vipaji vinavyoibuliwa ndani ya mashindao hayo lazima uendelezwe ili kupata wanamichezo bora watakakidhi kiwango cha Kitaifa na Kimataifa.

Balozi Seif alisema mashindano ya Tamasha la Shirikisho la Zahilfe ni mwanzo wa kuelekea njia sahihi ya kupata vipaji hivyo sambamba na kuchangamsha akili za Wanafunzi katika kukabiliana vyema na masomo yao ya kila siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Sera ya Michezo Zanzibar ya Mwaka 2007 imeweka umuhimu wa kuimarisha Sekta ya Michezo Vyuoni na Maskulini Unguja na Pemba.

Alisema Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} kupitia Sera hiyo kimeanzisha mafunzo maalum yalaiyowezesha kutoa Wahitimu 9 wa Stashahada ya Michezo ambao tayari wameanza kusomesha katika maskuli mbali mbali Nchini.

Balozi Seif alihimiza umuhimu wa kuimarishwa michezo Maskulini na Vyuoni kwa vile inasaidia kupatikana kwa matokeo mazuri ya Wanafunzi hasa kwenye mitihani yao pamoja na kuimarika kwa nidhamu miongoni mwa wanafunzi na walimu wao.

Alisema nidhamu inamuwezesha mtu sio mwanafunzi pekee kufanya kazi zake kwa mipango maalum na akafarajika na utaratibu wa kuanzishwa kwa mashindano ya Zahilfe yatakayofungua njia sahihi ya kudumisha nidhamu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo na Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali Zanzibar kwa jitihada za watendaji wake kuwaweka pamoja Wanamichezo hapa Nchini.

Mapema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pemba Juma ameipongeza Benki ya Biashara ya NMB kwa moyo wa kizalendo wa kuamua kwa makusudi kusaidia Sekta ya Elimi Visiwani Zanzibar.

Waziri Riziki alisema Benki ya NMB mbali ya kusaidia Sekta ya Michezo lakini pia juhudi zake za kusaidia Kompyuta 50 pamoja na Vikalio 450 kwa Skuli za Zanzibar ni ushahidi wa wazi unaothibitisha kwamba Uongozi wa Benki hiyo unaendelea kujali umuhimu wa Sekta ya Elimu inayofinyanga wataalamu wa fani zote.

“ Benki ya NMB imekuwa mshirika mkubwa wa Sekta ya Elimu Nchini, mbali ya kusaidia michezo lakini pia kuongeza nguvu zake katika kupunguza uhaba wa Vikavio na vifaa muhimu maskulini kama Kompyuta”. Alisema Waziri wa Elimu Zanzibar.

Akitoa salamu katika uzinduzi huo wa Tamasha la Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} Afisa Mkuu Wateja wadogo wadogo na wa kati pamoja uendeshaji Matawi ya Benki ya NMB Bwana Abdulmajid Nsekela alisema Taasisi hiyo ya kifedha itaendelea kusaidia huduma za Kijamii kadri mapato ya makusanyo yake yanavyoongezeka.

Bwana Nsekela alisema wadau wakuu wa Taasisi hiyo wengi wao ni Wananchi, hivyo hakuna budi wala kigugumizi kwa Uongozi wa Benki hiyo kuzipa kisogo changamoto zinazowakabili Wananchi hao katika maeneo yao wanayoishi.

Hilo ni Tamasha la Tano la Michezo inayoandaliwa na Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE} tokea kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2013.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/5/2017.

Thursday, 20 April 2017

BALOZI WA MPYA WA CUBA AJITAMBULISHA KWA DK.SHEIN


ZA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha.

ZA 1
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha.
ZA 2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo (katikati) wakiwa katika mazungumzo wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha, (kushoto) Mke wa Balozi Bibi. Meylin Suarez pia Afisa Mkuu wa Mambo ya Nje,daraja la Pili (kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (GAVU).
ZA 3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na mgeni wake Balozi mpya wa Cuba katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Lucas Domingo Hermandez Polledo (kushoto) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha kwa Rais, (kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (GAVU),[Picha na Ikulu.] 19/04/2017.

Saturday, 1 April 2017

DK. SHEIN AFUNGUA SEMINA YA SIKU MOJA YA VIONGOZI NA WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO VYA SERIKALI ZANZIBAR


A
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.
A 1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.
A 2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud mara alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika Semina ya Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo.
A 3
Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Rashid Ali Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika wengine alipowasili katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.
A 4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi na Waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.
A 5
Baadhi ya Wahariri wa Habari na waandishi wa habari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.
A 6
Wakuu wa Wilaya za Zanzibar na Waandishi wa habari wakiwa katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
A 7
Washauri wa Rais wa Zanzibar ni mongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika Semina ya siku moja ya Viongozi na Waandishi wa Habari wa Vyombo vya Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
A 8
Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja.
A 9
Baadhi ya Wanahabari wa Vyombo vya Serikali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wanahabari hao katika Semina ya siku moja iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja 01/04/2017.

Picha na Ikulu.

Thursday, 26 January 2017

BALOZI SEIF ATEMBELEA JENGO LILILOPOROMOKA MJI MKONGWE


Eneo la juu la nyumba ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar iliyopo Hurumzi ambalo lililonyofoka upande wa mbele na kusababisha kifo cha Mtu Mmoja aliyekuwa miongoni mwa Mafundi Wanne waliokuwa wakiendelea na matengenezo makubwa ya Nyumba hiyo

Nyumba ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ikionekena kuharibika vibaya baada ya ukuta we mbele kunyofoka mapema asubuhi ya Jumatano wakati mafundi wakiwa kazini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akiangalia nyumba ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana iliyoporomoka ukuta wa mbele baada ya kufanya ziara fupi ya kuangalia mkasa huo uliosababisha kifo cha Mtu Mmoja.

Balozi Seif wa Pili kutoka Kushoto akimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makarani wa kwanza kushoto kufanya ukaguzi wa Nyumba zilizomo ndani ya Mjui huo ili punguza maafa yanayoweza kuepukwa mapema.


Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Nd. Marina Joel Thomas. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Mamlaka ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar kuandaa mpango maalum utakaoshirikisha Taasisi nyengine husika kwa ajili ya kuzifanyia ukaguzi wa mara kwa mara nyumba zote zilizomo ndani ya Mji huo.

Alisema mpango huo wa Kitaalamu utaweza kutoa muelekeo wa kina kwa kuzitambua nyumba zote zilizochakaa na ambazo kwa mazingira ya Mji huo haziwezi tena kuhudumia makaazi ya Wananchi wake.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo mapema asubuhi alipofanya ziara fupi ya kulikagua Jengo la Ghorofa Tatu la Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana katika Mtaa wa Hurumzi ndani ya Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya kuporomoka wakati mafundi wakiwa katika harakati za kulifanyia matengenezo makubwa.

Maporomoko hayo yaliyomfunika Fundi Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Khamis Kombo yalisababisha kifo chake kilichothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi na Fundi mwengine kulazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja baada ya kujeruhiwa vibaya.

Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kamwe haitovumilia kuona Wananchi wake wanaendelea kuishi katika mazingira hatarishi ndani ya nyumba ambazo itathibitishwa na Uongozi na Wataalamu hao wa Mamlaka ya Mji Mkongwe kwamba hazistahiki kuishi Wanaadamu.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makarani alisema Uongozi wa Mamlaka hiyo pamoja na ule wa Shirika la Nyumba Zanzibar uko katika hatua ya mwisho ya kufanya mazungumzo ili Wataalamu wake wafanye zoezi maalum la kuzikagua nyumba zote za Serikali zilizomo ndani ya Mji huo.

Nd. Sarboko alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba zoezi hilo litabainisha wazi Ngumba zilizoharibika kabisa na kuwa katika mazingira hatarishi jambo ambalo juhudi za makusudi zitachukuliwa katika kuona lile fungu dogo la fedha linalopatikana lielekezwe katika kuziokoa kwanza nyumba hizo.

“ Tunatarajia kuwa na zoezi la pamoja kati yetu sisi watu wa mamlaka ya Mji Mkongwe na wenzetu wa Shirika la Nyumba Zanzibar kuzikaguwa ili tuzitambue nyumba za Serikali zilizo katika hali mbaya na baadaye kuzifanyia matengenezo ya dharura ”. Alisema Nd. Issa Sarboko Makarani.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud alisema Uongozi wa Serikali ya Mkoa wake hautokubali kuridhia malalamiko yanayotolewa na yatakayoendelea kutolewa na baadhi ya watu dhidi ya Serikali kwa uamuzi wake wa kuhami maisha ya wananchi wake.

Mheshimiwa Ayoub alisema jambo la msingi litakaloendelea kuchukuliwa na kutiliwa mkazo na Serikali ni dhima ya kuhami uhai wa maisha ya Raia wakati panapojitokeza dalili za maafa bila ya kujali kasumba za kisiasa zinazopigiwa debe na baadhi ya watu wakiwepo pia wanasiasa.

Ujenzi wa jengo hilo la Ghorofa Tatu Mali ya Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar ulikuwa unafanyika kwa mujibu wa sheria na taratibu zote za mamlaka ya Uhifadhi na Utunzaji wa Mji ya mkongwe wa Zanzibar.

Kikosi cha zimamoto na Uokozi Zanzibar kilifika katika eneo la tukio mara baada ya kuanguka kwa ukuta wa mbele wa Nyumba hiyo na kujaribu kumuokoa fundi aliyefukiwa na kifusi ambae tayari alikuwa ameshafariki Dunia na maiti yake kupelekwa hospitali kuu ya Mnazimoja kwa uchunguzi kabla ya kukabidhiwa familia kwa ajili ya mazishi.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/1/2017.

Wednesday, 11 January 2017

KUELEKEA MIAKA 53 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, BALOZI SEIF ASHUHUDIA MATAYARISHO YA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA UWANJA WA AMAN

Kikosi cha Bendera cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikikamilisha mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kilele cha sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar hapo uwanja wa Aman Mjini Zanzibar.
Makamanda wa JWTZ Wanawake wakati walipotoa heshima yao kwa mwendo wa pole kwenye zoezi la mwisho la matayarisho ya kilele cha sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vikosi vya ulinzi na usalama vikienda mwendo wa hatua 15 katika Uwanja wa Aman wakikamilisha mazoezi yao ya mwisho kwa ajili ya Kilele cha sherehe za Mapinduzi Januari 12, 2017.
Vijana wa Dr. John Pombe Magufuli (Makomandoo) wakifanya vitu vyao wakati wa mazoezi yao ya mwisho wakijiandaa na kilele cha sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiiongoza Kamati yake katika kufanya tathmini ya Gwaride la maandalizi ya sherehe za Mapinduzi kutumia miaka 53.
Wajumbe wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa wakiendelea na kikao chao hapo ukumbi wa watu mwashuhuri { VIP }Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Nd. Omar Hassan Omar wakikagua ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi hapo Kikiwajuni ulioandaliwa kwa ajili ya Taarab Rasmi ya Kukamilisha sherehe za Mapinduzi.
Balozi Seif akielezea matumaini yake ya kukamilishwa kwa wakati matayarisho ya ukumbi huo. Picha na OMPR – ZNZ.

                                                                                      Na Othman Khamis Ame, OMPR
Wakati shamra shamra za sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zikikaribia hatua ya ukingoni katika maeneo mbali mbali hapa Nchini, matayarisho ya mwisho ya kilele cha maadhimisho hayo kwa upande wa Vikosi vya ulinzi na usalama yamekamilika.

Matayarisho hayo ya mwisho yalijumuisha gwaride rasmi la Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Polisi, Mafunzo, KMKM, JKU, Magereza, Valantia na Zimamoto na Uokozi yakiambatana na vikundi vya Utamaduni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif Ali Iddi alijumuika pamoja na Makamanda wa Vikosi na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kushuhudia matayarisho ya vikosi hivyo kwenye uwanja wa Aman Mjini Zanzibar.

Askari wa Vikosi hivyo wakiwa makini na hali ya Ukakamavu waliweza kupita mbele ya Mwenyekiti huyo na wajumbe wake kwa mwendo wa pole na ule wa haraka ulioleta burdani safi kwa watazamaji hao.

Wazanzibar na Watanzania wote mwaka huu watashuhudia Kwata maalum ya kimya kimya iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambayo ilikuwa gumzo wakati wa mazoezi yao ya mwisho wakijiandaa na Kilele cha maadhimisho hayo ya kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya maandalizi hayo hapo ukumbi wa Watu mashuhuri Uwanja wa Aman Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif Ali Iddi amepongeza kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Wananchi, Viongozi pamoja na Vikosi vya ulinzi katika maandalizi ya sherehe za mwaka huu.

Balozi Seif alisema Viongozi wa Serikali wanazidi kufarajika kuona kwamba ushiriki wa Wananchi katika kuziendeleza sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 unazidi kuongezeka mara dufu.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliangalia Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi uliopo Kikwajuni Mjini Zanzibar kuangalia matayarisho ya mwisho kwa ajili ya Taarab rasmi na kukamilisha maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 53.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Nd. Omar Hassam Omar alimueleza Balozi Seif kwamba watendaji wa idara ya Sanaa na Utamaduni wanasubiri maelekezo ya wataalamu wa mapambo kukamilisha kazi iliyobaki ya upambaji Ukumbi huo.


Nd. Omar alisema licha ya udogo wa Ukumbi huo lakini mipango iliyoandaliwa kwa ajili ya Taarab hiyo inakwenda vyema ikiwemo kadi maalum zilizoandaliwa kwa burdani hiyo ya Taarab.
Kilele cha sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 53 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Aman asubuhi ya Alhamisi ya Tarehe 12 Januari 2017.

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA