CHONDE CHONDE UKAWA RUDINI BUNGENI.....PINDA ASEMA
Dodoma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewasihi viongozi wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kurejea katika vikao vya Bunge Maalumu la Katiba
vinavyotarajiwa kuendelea tena kuanzia Agosti 5 mwaka huu.Amesema
kama tatizo la wajumbe wa umoja huo kususia vikao vya Bunge hilo wiki
moja kabla ya kuahirishwa kwake ni kejeli na matusi kama ilivyoelezwa na
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe, jambo hilo linazungumzika.Waziri
Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati wa kuhitimisha na kutoa ufafanuzi
wa hoja mbalimbali za wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya ofisi
yake kwa mwaka 2014/15.Mei
7 mwaka huu, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni wakati akitoa hotuba yake kuhusu Bajeti ya Waziri Mkuu, alisema
wajumbe wa Ukawa hawatarejea katika Bunge la Katiba mpaka
watakapohakikisha kuwa maana halisi ya uwepo wa Bunge hilo unafuatwa.
Alisema
kama lengo ni kutumia mwamvuli wa Bunge Maalumu la Katiba ili
kuendeleza mfumo wa kikatiba na muundo wa muungano uliopo sasa, wajumbe
wa Ukawa hawatakuwa sehemu ya usaliti huo kwa Watanzania, huku
akisisitiza kukerwa kwake na lugha za matusi na kejeli dhidi yao
zilizokuwa zikitolewa na wajumbe kutoka chama tawala.
Hata hivyo Pinda jana alisema “Kauli zilizotolewa na Mbowe zilikuwa kali
na zilinitisha kidogo. Nadhani tusianze kutoa picha kwa Watanzania juu
ya hali ya kutokuwepo kwa amani katika siku zijazo kwa sababu jambo
hili siyo zuri,” alisema Pinda na kuongeza;
“Nadhani kubwa hapa ni kuendelea kuzungumza juu ya uwezekano wa namna ya kufikia hatima nzuri juu ya mchakato wa Katiba.”
Pinda alisema sababu za lugha za kejeli na matusi zilizotolewa na Mbowe
siyo sababu ya msingi ya kuwafanya wajumbe wa Ukawa kususia vikao vya
Bunge hilo.
“Hata kama tungefikia mahali tukavutana sana, suluhu haikuwa kutoka nje
ya Bunge. Hata kama mngesema liahirishwe ili tukajadiliane na
kukubaliana na kisha kurejea na kuendelea na mjadala, sidhani kama
lingekuwa tatizo.”
Waziri Pinda alisema Rais Jakaya Kikwete hakuwa chanzo cha kuvuruga
mchakato wa Katiba kama ilivyoelezwa na Mbowe na kufafanua kuwa Rais
Kikwete kama wananchi wengine naye alikuwa akitoa maoni yake na kwamba
alieleza wazi kuwa wabunge ndiyo wenye uamuzi wa mwisho.
uku akiwataja wajumbe kadhaa wa Ukawa, Pinda alisema: “Bado naamini
Mbowe, James Mbatia, John Cheyo na Profesa Ibrahim Lipumba tunaweza
kuzungumza, maana kama hoja ni matusi na kejeli, hivi tukikubaliana si
tunarudi na kukubaliana kutokuwapo kwa vitu hivyo.”
Alisema kuwa anaunga mkono kauli ya Mbowe ya kukutanisha makundi yote yanayopingana ili kuzungumza ili yaweze kukubaliana.
0 comments:
Post a Comment