Hatari nyingine mpya ya bakteria kwenye ndege za kusafiria
Ripoti
imetolewa ikionyesha sehemu gani ndani ya ndege inalea vijidudu vya
bakteria zaidi ikiwemo ile sehemu ya kuwekea mkono katikati ya viti,
kwenye vidirisha pamoja na sehemu ya nyuma ya kiti panapotumika kuweka
vitu mbalimbali.Wachunguzi wa Chuo cha Auburn nchini Marekani wamefanya
uchunguzi ili kujua ni sehemu gani ndani ya ndege inalea na inaruhusu
vijidudu vinavyosababisha maambukizo ya magonjwa mbalimbali likiwemo
gonjwa kali ya E.Coli.Uchunguzi waliufanya ndani ya ndege ya Delta
Airlines ambayo hufanya safari zake nchini humo.
Bakteria
anaesababisha ugonjwa wa E.Coli ambao bado sijapata maelezo yake ya
kitaalamu jinsi unavyoathiri mwili wa mwanadamu, anaweza kuishi mpaka
siku 7 kwenye meza za kulia chakula ndani ya ndege ambapo kwa kipindi
hiki unaambiwa ni hatari na kwa binadamu na ndio anatumia hiyo time
kuusambaza.
Wachunguzi
hao wameshauri watu kunawa mikono mara kwa mara na kutumia dawa za
kusafishia mikono ambazo zinatumika kuulia bacteria yaani
anti-bacterial.
NA MATUKIO BLG
0 comments:
Post a Comment