HII NI LAANA MJUKUU AMBAKA NA KUMLAWITI BIBI YAKE
Bibi anayesadikiwa kibakwa na kulawitiwa na mjukuu wake aliyefahamika kwa jina moja la Pius.
UNYAMA
uliyoje! Kijana aliyefahamika kwa jina moja la Pius (28), mkazi wa
Kijiji cha Nyingwa Kata ya Kibungo Juu, Tarafa ya Matombo wilayani
Morogoro Vijijini, anasakwa kwa tuhuma za ubakaji na ulawiti wa bibi
mmoja,(74).Kwa mujibu wa chanzo chetu, mtuhumiwa huyo alikamatwa na
kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Tawa wilayani humo, lakini
alitoroka akiwa amefungwa pingu saa chache baada ya kufikishwa kituoni
hapo.
Ilidaiwa kuwa bibi huyo ambaye alikuwa msibani alitendewa unyama huo wakati anarejea nyumbani kwake.
Taarifa
zilidai kuwa baada ya kutendewa unyama huo na kuharibika vibaya sehemu
nyeti, bibi huyo alipelekwa katika Zahanati ya Tawa, lakini akahamishiwa
kwenye Hospitali ya Rufaa Morogoro kwa matibabu zaidi.
Akizungumza
na mwanahabari wetu, mtoto wa bibi huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Novitha Martin alidai kuwa Pius ndiye aliyemfanyia unyama mama yake.
”Baada
ya kumbaka na kumlawiti, mwenyekiti wetu wa Kijiji cha Nyingwa, Roman
Deli kwa kushirikiana na mgambo wa kijiji walifanikiwa kumkamata
mtuhumiwa usiku huohuo na kumfunga kamba.
“Alilala
kwa mwenyekiti hadi kulipokucha Aprili 21 mwaka huu, akasafirishwa hadi
Kituo cha Polisi Tawa na kufungua jalada la kesi namba
TAW/RB/33/2014-UBAKAJI kisha akapewa PF-3 aliyoitumia kwenye matibabu
katika Zahanati ya Tawa,” alisema Novitha.
Mwandishi
wetu alifika Kituo cha Polisi Tawa ambapo askari wa zamu alisema hawezi
kuzungumza chochote kwa kuwa yeye siyo msemaji wa jeshi hilo.
Alipofika
katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na kuzungumza na Mganga Mkuu
Msaidizi, Dk. Nuhu Muhinge, alikiri kumpokea bibi huyo akiwa katika hali
mbaya.
Kwa upande wake bibi huyo aliyetendewa unyama, alisema:
“Nilipofika
kwenye kichaka wakati narudi nyumbani alinipiga ngwara, akanivua nguo
kisha alinifanyia tendo ambalo niliacha kulifanya zaidi ya miaka 15
iliyopita, aliniteka na alianza kunibaka saa kumi jioni hadi saa mbili
usiku.
“Aliponiachia
nilijikongonja hadi kwenye kigango cha kanisa letu la Katoliki Kigango
cha Gomelo ndipo nilipata msaada wa hifadhi na kutoa taarifa kwa
mwenyekiti wetu wa kijiji.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alipohojiwa na mwandishi
wetu kuhusiana na tukio hilo alisema halijatumwa ofisini kwake.
”Ngoja
nimwite OCD awasiliane na mkuu wa Kituo cha Tawa, acha namba zako za
simu tukilikamilisha tutakupigia,’’ alisema kamanda huyo ambaye amehamia
mkoani hapa Jumanne iliyopita akitokea Mkoa wa Geita akiziba nafasi ya
Faustine Shilogile aliyehamishiwa makao makuu ya polisi jijini Dar.
NA GLP
0 comments:
Post a Comment