Watatu wauawa kwa bomu Mombasa
Watu watatu wanaripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea katika mji wa Mombasa nchini Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono lilitupwa kwenye basi katika kituo cha mabasi cha Mwembe Tayari.
Mlipuko
mwingine umetokea katika mtaa wa kifahari wa Nyali.ambalo hupendwa
kutembelewa na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.
Kamishna
mkuu wa polisi Mombasa, Nelson Marwa, watu 6 wamejeruhiwa na kuwa watu
waliotekeleza shambulizi hilo walitoroka kwa Pikipiki.
Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la nchini Somalia.
Aidha
nchi hiyo imekuwa katika tahadhari tangu mwezi Septemba mwaka jana
ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia kituo cha biashara cha Westgate
kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu wapatao 67.
Al
Shabaab ni kundi ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda
ambalo limeapa kulipiza kisasi kufuatia Kenya kutuma majeshi yake nchini
Somalia mwaka 2011ambayo yameungana na yale ya Umoja wa Afrika AMISOM.
0 comments:
Post a Comment