Kutana na jamaa kutoka Kenya aliyeamua kujifunga mnyororo kwenye mnara wa shujaa Kimathi.
07:56 | No Comments |
Unaambiwa kuna jamaa mmoja kutoka Nairobi amesababisha baadhi ya shughuli kusimama kwa saa kadhaa kwenye barabara ya Dedan Kimathi kwa kuamua kujifunga minyororo kwenye Mnara wa shujaa huyo wa kupigania uhuru wa Kenya akidai kwamba yeye ni mjukuu wa kimathi ambaye ndiye sanamu yake iliyowekwa.
Kwenye picha ni maafisa wa Baraza la Jiji la Nairobi waliokuwa wanamzubaisha ili ajifungue na kushuka chini hata hivyo jamaa amekataa kujifungua kutoka kwenye Mnara mnara huo anaodai ni wa babu yake.
0 comments:
Post a Comment