HALI YA MWANASOKA PELE MATATANI,ALAZWA ICU
Mchezaji wa siku nyingi nchini Brazil na aliyeiwezesha Brazil kunyakua kombe la Dunua mara tatu amelazwa hospitali ya mjini Sao Paulo kwa maambukizi baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa mawe kwenye figo ya mchezaji huyo.
Pele mwenye miaka 74 alilazwa kwenye hospitali hiyo jumanne wiki hii baada ya kupata maambukizi kutokana na kufanyiwa upasuaji kuondoa mawe kwenye figo mwezi uliopita.
Madaktari wa hospitali ya Albert Einstein ya mjini Sao Paulo wamesema hali ya mchezaji huyo inaendelea kuimarika lakini habari kutoka kwa shirika la habari la AFP zinasema hali ya mchezaji huyo inaendelea kuwa mbaya amewekwa chini ya uangalizi maalum kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.