KOCHA JUMA MWAMBUSI WA MBEYA CITY AJIUZULU
20:34 |
Ripoti kadhaa ambazo hazijathibitishwa na uongozi wa mbeya city zinasema kuwa kocha wa timu hiyo Juma Mwambusi amejiuzulu .
Hatua hiyo imekuja baada ya kuishuhudia timu yake ikipata mfululizo wa matokeo mabaya kwenye ligi ambapo katika michezo saba imeweza kushinda mchezo mmoja pekee huku ikitoka sare kwenye michezo miwili na kufungwa jumla ya michezo minne .
Taarifa mbalimbali toka jijini Mbeya zinasema kuwa kwa muda mrefu wachezaji wa Mbeya City walikuwa wamepoteza Imani na kocha wao hali ambayo mashabiki wanaamini kuwa imechangiwa na pengo la aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo Maka Mwalusi .
Mwalusi ambaye alihama Mbeya City na kwenda kuifundisha timu ya ligi daraja la kwanza ya Panoni Fc ya mjini Moshi anadaiwa kutoridhishwa na kitendo cha kupewa ‘mgao kiduchu’ wa zawadi ya kocha bora ambaye bosi wake Mwambusi aliipata hali ambayo ilionyesha kutothaminiwa kwa mchango wake .
Hali ya Juma Mwambusi ilikuwa inaonekana kuwa mbaya kadri Mbeya City ilivyozidi kupata matokeo mabaya hasa baada ya kujikuta ikipoteza michezo minne mfululizo mbele ya timu za Azam Fc , Mtibwa Sugar , Mgambo Jkt na Stand United.
Endapo taarifa hii itathibitika kuwa Kweli Mwambusi ambaye msimu uliopita alitwaa tuzo ya kocha bora wa msimu kabla ya kutwaa tuzo nyingine ya kocha bora wa mwezi septemba wakati ligi ilipoanza atakuwa kocha wa pili kupoteza kibarua chake baada ya Denis Kitambi ambaye alifukuzwa kazi na Ndanda Fc baada ya matokeo mabaya .
Related Posts:
MESSI APIGA MBILI BARCELONA IKIIADHIBU EIBAR 4-0 Nyota wa Barcelona, Lionell Messi (kulia) akifumua shuti kuifungia bao la pili timu yake katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Eibar kwenye mchezo wa La … Read More
CHELSEA YAPETA LIGI KUU ENGLAND Diego Costa wa Chelsea akiushuhudia mpira ukitinga nyavuni baada ya kumchambua kipa wa Norwich katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jum… Read More
WAMEPIGWA!!! MANCHESTER UNITED YATULIZWA NA WEST BROM, 1-0 Nyota wa West Bromwich Albion, Salomon Rondon akifumua shuti huku beki wa Manchester United, Chris Smalling akijaribu kuzuia katika mchezo wa Ligi… Read More
SIMBA YAITUMIA MBEYA CITY KAMA NGAZI KUPANDA KILELENI MWA LIGI Awadh Juma na Daniel Lyanga kulia wakishangilia na Ibrahim Hajib aliyepiga magoti baada ya kufunga bao la pili dakika ya 90. Kushoto ni kipa wa M… Read More
LIVERPOOL YALIPA KISASI KWA KUITANDIKA MAN CITY TATU BILA Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino akimrukia migongoni mshambuliaji wa Liverpoool, Divock Origi wakati wakimpongeza James Milner baada ya… Read More