Tuesday, 16 December 2014

THIERRY DANIEL HENRY ATANGAZA KUSTAAFU SOKA



henryThierry Daniel Henry alizaliwa August 17, mwaka 1977 ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa ambaye leo hii ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka akiwa na klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki ligi kuu ya Marekani maarufu kama Major League Soccer.

hen
Henry alizaliwa Les Ulis, Essonne kitongoji kilichopo Paris nchini Ufaransa toka akiwa mdogo alitajwa kama atakuja kuwa mshambuliaji bora .
Alisajiliwa na AS Monaco mwaka 1990, alianza kucheza soka la kulipwa mwaka 1994,kwa mara ya kwanza aliitwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa mwaka 1998, enzi hizo anacheza kwenye ligi kuu ya Serie A , akiwa na mabingwa wa wakati huo timu ya Juventus.
Hakuwa na msimu mzuri , enzi hizo akiwa anacheza winga , kabla hajajiunga na klabu ya Arsenal kwa ada ya paun milioni 11 mwaka 1999.
Akiwa na Arsenal Henryalipata umaarufu mkubwa kiasi cha kutajwa kuwa ni mmoja ya wachezaji mahiri waliowahi kutikisa kwenye ulimwengu wa soka.
Japo mwanzoni alipata shida kwenye Premier League, lakini akaja kuwa mmoja ya washambuliaji wa wakati wote wa klabu ya Arsenal.
Chini ya kocha Arsène Wenger, Henry alifunga magoli 228 kwenye michuano yote na kuwa mshambuliaji mwenye mabao mengi kwenye historia ya washika bunduki wa jiji la London.
henr
Henry alitwaa mataji mawili ya ligi kuu ya England , mataji matatu ya FA akiwa na Arsenal , aliwahi kushika nafasi ya pili kwenye tuzo ya mchezaji bora wa wa dunia wa FIFA ma mbili , pia amewahi kutwaa tuzo mbili ya mchezaji bora wa mwaka nchini England, pia mchezaji bora wa mwaka anachaguliwa na wachezaji wenzie mara tatu.
Miaka miwili ya mwisho ya Henry akiwa Arsenal alikuwa nahodha wa wa timu hiyo, aliiongoza Arsena kucheza fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2006.
June mwaka 2007, baada ya kuichezea Arsenal, kwa miaka nane alijiunga na Barcelona kwa ada ya paun milioni 24. Mwaka 2009, alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kilichotwaa mataji matatu La Liga, Copa del Rey pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Aidha akiwa na Barcelona alifanikiwa kutwaa taji la Supercopa de España, pia UEFA Super Cup pia FIFA Club World Cup.
Henry alitajwa kwenye kikosi cha timu bora ya mwaka ya mara tano. Mwaka 2010, alijiunga na klabu ya New York Red Bulls inayoshiriki Major League Soccer ya nchini Marekani, walifanikiwa kutwaa taji la Eastern Conference mwaka 2010. Alirejea Arsenal kwa mkopo wa miezi miwili mwaka 2012. Mwaka 2013 Henry akiwa na New York Red Bulls alitwaa tuzo wa mashabiki wa MLS ijulikanayo kwa jina la ngao.

Henryaliwahi kupata mafanikio akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, alikuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 1998 , pia alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa taji la UEFA Euro mwaka 2000 na taji la kombe la mabara mwaka 2003.
October mwaka 2007, alivunja rekodi ya gwiji Michel Platini kwenye timu ya taifa ya kwa kuwa mfungaji wa wakati wote timu ya taifa hilo.

henryy
Henry alistaafu soka la kimataifa mwaka 2010 baada ya fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini. Nje ya uwanja, Henry ni msemaji wa masuala ya ubaguzi wa rangi kwenye mpira wa miguu,hiyo inatoka na kuwa muhanga wa matukio ya namna hiyo. Alimuowa mwanamitindo wa England Nicole Merry mwaka 2003 wana mtoto mmoja wa kike , ingawa wawili hao walipeana talaka mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA