Sunday 23 January 2022

ZIJUE AINA 10 ZA WANAWAKE WANAOPENDWA SANA NA WANAUME



WAPENDA USAWA-
Hii ni aina ya kipekee inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu yakifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50

WANAOJUA MAPENZI-
Wanawake wajuzi wa mambo ya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa niuwezo wa kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha kuwa wanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume bila kujali sifa zao za nje au za ndani.

MARAFIKI -
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume.Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida naraha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na wapenda amani.

WAPENDA UWAZI-
 Aina nyingine ya wanawake inayowavutia wanaume ni wenye msimamo nawapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika maamuzi ya msingi kwakisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti unaonesha wanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye tabia za ubabe na udhaifu katikauelewa wa mambo. 

WANAOJITEGEMEA-
 Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza stareheza upande mmoja. 

WASIO NA PRESHA-
Nikisema wanawake wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe nakazi yao kuwa ni kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi

MARIDADI-
 Kundi lingine la wanawake wanaopendwa na wanaume ni wanaozingatia usafi
na kujiremba. Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa mwonekano. 

WANAORIDHIKA-
 Wanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.

WA MMOJA-
 Wanawake wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana.“Niliye naye ananitosheleza kwa kila kitu sitaki mtu mwingine.”Kundi la wanawake wa aina hii ni adimu na muhimu sana.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA