Monday 9 March 2015

DARUBINI YA AFANDE::MAKALA

Image result for darubini

Nakumbuka miaka ya nyuma msaani mmoja anaitwa Afande sele alitoa nyimbo yake inaitwa daruni na kitiko cha nyimbo hiyo kilisema "Ni mimi msaani ,ni mimi msaani ni mimi kioo jamii ni mimi naona mbali kwa darubini kaili".


Leo ningekuwa msaani ningeuza wimbo huu na kusema "Ni mimi kijana,ni mimi kijana kioo cha jamii ni mimi naona mbali kwa darubini kali".Kila nifikiria hapo vijan huwa nasema ndio kioo ch jamii na ndio wanaoyakiwa kuona mbali.


Lazima ifike hatua tuseme vijana wanaweza kututoa hapa tulipo kama watajua jukumu lao ni nini na vijana wanaweza kututoa hapa tulipo kama watafanya wajibu wao wa msingi.


Jamii ina mtazamo kuhusu vijana wakati mwingine vijana wanaonekana kama watu wasio tambua wajibu wao na vijana wengiene wanatenda mambo kama wao sio kioo cha jamii hakuna njia nyingine zaidi ya kusema mimi ni kijana lazima nionyeshe mfano wa kuigwa.

Leo hii tunajivunia juhudi na mipango ya watu wengine kwa sababu walijua wao ni kioo cha jamii na waliona mbali wakatekeleza jukumu lao la kuona mbali.

Sote tunajua ujasiri wa Mkwawa,Mwalimu Nyerere,Sokoine na wengine wengi ni kwa sababu walijuwa wao ni vijana wanatakiwa kuwa kioo na kuona mbali.

Wewe kijana maisha yako ya leo ndio yanatoa uhalisia wa juhudi zako za kuitoa jamii hapa ilipo kwenda hatua nyingine.Ni muhimu kutambua kuwa ujana huja na kupita .

Kizazi cha 2015 kitakubukwa kwa juhudi zake za kutenda na kusimamia mambo ila vijana ndio wanataakiwa kuwa mstari wa mbele maana wao ndio wanatakiwa kuona mbali zaidi.

Ni malizie kwa kusema kijana ni kioo ch jamii na kijana anatakiwa kuona mbali kwa darubini kali.

-kiduo mgunga <kmgunga@gmail.com

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA