Monday, 9 March 2015

MIPANGO KUMDHURU DK. SLAA YAFICHUKA

Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, Khalid Kangezi, anahojiwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, kwa tuhuma za kushiriki katika mipango ya kukihujumu chama hicho na kutaka kumdhuru Dk. Slaa. Taarifa za awali zilizotolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, mbele ya waandishi wa habari, zilieleza kuwa Kangezi amekuwa akitumiwa na maofisa 22 wa vyombo vya usalama katika miaka miwili iliyopita kufanya mipango hiyo dhidi ya chama hicho. Marando alidai mipango hiyo imegunduliwa na kitengo cha usalama cha Chadema kupitia simu za Kangezi na kwamba, ililenga kuiumiza Chadema kisiasa. Alidai katika hujuma hizo, Kangezi amekuwa akiwasiliana na mmoja wa vigogo wa ngazi ya taifa wa CCM. Marando alidai kuanzia Desemba, mwaka jana hadi wiki iliyopita, Kangezi alikuwa amekwishafadhiliwa Sh. milioni saba kwa ajili ya matumizi ya mawasiliano ya simu kufanikisha upatikanaji wa taarifa za Chadema kupitia vikao vyake mbalimbali, ikiwamo kamati kuu. Alidai alipohojiwa na chama, Kangezi aliwapa kitabu chake cha kutunza kumbukumbu, ambacho kinaonyesha mawasiliano kati yake na baadhi ya maofisa wa vyombo vya usalama, aliowataja kwa majina na namba za simu zao za mikononi.
-EAST AFRICA RADIO

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA