Sunday 22 March 2015

JESHI LA KENYA NA AMISON WATEKA BANDARI KUTOKA KWA AL-SHABAAB


Jeshi la Ulinzi Kenya (KDF) pamoja na vikosi vya kulinda amani vya Somalia vilivyo chini ya mwavuli wa AMISOM vimeutwaa mji muhimu wa bandari kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini na Kanali David Obonyo, imesema operesheni hiyo kubwa katika fukwe imefanywa leo majira ya saa kumi alfajiri, ambapo wapiganaji kadhaa wa Al-Shabaab wameuwawa.

Wakati huo huo, magari ya kundi hilo matano yanayotumika kwa mikakati ya kivita yameharibiwa na shehena ya silaha zao kukamatwa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA