Sunday 22 March 2015

STEVEN GERRAD ACHEZA SEKUNDE 40 TU NA KUPEWA KADI NYEKUNDU, ROONEY AKOSA PENATI WAKATI MAN UNITED IKIITANDIKA LIVERPOOL 2-1


BONGE LA GOLI!!! Mshambuliaji wa Manchester United, Juan Mata akifunga goli la pili katika dakika ya 59 dhidi ya Liverpool katika mchezo uliomalizika kwa Manchester United kushinda 2-1. 

Timu ya soka ya Liverpool leo imejikuta ikikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa mashetani wekundu, Manchester United, katika mchezo ulioshuhudia nahodha wa Liverpool, Steven Gerald akicheza sekunde 40 tu ya kipindi cha pili na kutolewa nje kwa kadi nyekundu. 

Gerald aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo, alimchezea rafu mbaya Herrera kwa kumkanyaga mguu. Pia katika mchezo huo, Manchester United walikosa penati, baada ya mlinda mlango wa Liverpool, Mignolet kupangua mpira huo wa penati iliyopigwa na Wyne Rooney.
Mshambuliaji wa Manchester United Juan Mata akifunga goli la kwanza dakika ya 14.
Mshambuliaji mwenye kasi wa Liverpool, Daniel Sturridge akiifungia timu yake bao katika dakika ya 69.
Nenda nje!! Nahodha wa Liverpool, Steven Gerald akionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo, Martin Atkinson baada ya kumchezea rafu mbaya naya makusudi Ander Herrera wa Manchester United kwa kumkanyaga mguu huku akiwa tayari ameshaucheza mpira.
Gwiji la kandanda, Pelle alikuwepo uwanjani hapo kuufuatilia mchezo huo baina ya Liverpool na Manchester United.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA