Friday 6 March 2015

PAPISS CISSE AKIRI KUMTEMEA MATE BEKI WA MANCHESTER UNITED JONNY EVANS


Mchezaji wa Newcastle United, Papiss Cisse amekiri kosa la shitaka alilofunguliwa na Chama cha Soka cha Uingereza (FA) la kumtemea mate beki wa Manchester United Jonny Evans.

Mshambuliaji huyo sasa anakabiliwa na uwezekano wa kufungiwa kucheza mechi saba, kwa kufanya kosa hilo katika mchezo wa jumatano ambapo Manchester United ilishinda 1-0 dhidi ya Newcastle.

Hata hivyo beki Jonny Evans, hajajibu mashtaka ya FA ambayo naye yanamkabili kwa kufanya kosa hilo la kumtemea mate Cisse. Hata hivyo Evans alishakanusha kumtemea mate Cisse kwa makusudi.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA