Monday 9 March 2015

SIMBA YAZIDI KUITESA YANGA..CHEKI PICHA ILIVYOIFANYA JANA.

Kikosi cha Simba.
Kikosi cha Yanga.
Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan akiwania mpira na Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Simba imeshinda bao 1 - 0 lililotiwa kimiani kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Danny Mrwanda akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba,Kessy Ramadhan wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Abdi Banda wa Simba (kulia) akiondoka na mpira huku akikabwa na kiungo Haruna Niyonzima wa Yanga.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' akizozana jambo na mwamuzi wa mechi ya Yanga na Simba, Martine Saanya.
Kipa wa Yanga, Ally Mustapha 'Barthez' akiudaka mpira huku akishuhudiwa na kiungo wa Simba, Ramadhani Singano (katikati) na beki wa Yanga, Oscar Joshua.
Beki wa Yanga, Mbuyu Twite akiondoa mpira huku akizongwa na Emmanuel Okwi wa Simba.
 Nyanda nambari moja wa timu ya Simba,Ivo Mapunda akiwa ametulia langoni kwake tayari kwa kuzuia shuti lililopigwa na Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva.
Wakati mtanage ukiendelea,ghafla likatokea zogo baina ya Nahodha wa Timu ya Yanga na Kiungo wa Simba,Abdi Banda na mambo yalikuwa hivi.
"Beki hasififiiiii lakini hapa anastahili sifa....",Beki wa Simba,Juuko Murshid akiruka juu kuondoa mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake,mbele ya Washambuliaji wa Yanga.
Kipa wa Yanga,Ally Mustafa "Bartez" akiwa ameruka juu kuondoa hatari langoni kwake.
Mshambuliaji wa Yanga,Simon Msuva akiangalia namna ya kumtoka Beki wa Simba.
Beki wa Simba,Kessy Ramadhan akimzungusha mshambuliaji wa Yanga.
Anacheza paleeeee Ivo Mapunda.
Haya nendeni kuleeeeee......
Wee kipa hili Taulo lako silitaki hapa,naliweka huku nje.
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akiachia nduki kali ambalo hata halikuzaa matunda.
Mashabiki wa Yanga wakijifariji.
Washabiki wa Simba wakiwabeza wenzao wa Yanga.
Wadau wa IMETOSHA wakiendelea kuwakilisha uwanjani.

Umati wa Washabiki wa Timu ya Simba ukiwa umefurika uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam kuipa sapoti timu yao ambayo haikuwaangusha leo,baada ya kuwatandika bao 1 - 0 watani zao wa jadi Yanga,lililotiwa kimiani kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji,Emmanuel Okwi mnamo dakika ya 52 ya mchezo.
Ulinzi ulikuwa ni wa uhakika kabisa.
Hatari lakongoni mwa timu ya Simbaaaaa....
Kadi Nyekunduuuuu kwa Mchezaji wa Yanga,Haroun Niyonzimaaaaa.... baada ya kupiga mpira ulioingia wavuni baada ya refa kupiga filimbi kuwa ni faulo.
Niyonzima anamzonga Mwamuziii
Mshambuliaji wa Yanga,Amis Tambwe akizungumza na Mwamuzi juu ya Kadi aliyopewa Niyonzima.
Ukiangalia vyema utabaini kitu

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA