Wednesday 1 April 2015

KESSY AFUNGUKA::SITAREJEA SIMBA SC HADI NILIPWE NA NIPEWE NYUMBA


Hassan ‘ Kessy’ RamadhaniNa Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Mlinzi wa kulia kwa klabu ya Simba SC, Hassan ‘ Kessy’ Ramadhani amejiondoa katika timu hiyo kwa sababu za klabu kushindwa kumpatia Nyumba ya kuishi huku pia akiendelea ‘ kupigwa dana dana’ kuhusu sehemu ya malipo yake ya usajili. Kessy alisaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro katika usajili wa dirisha dogo mwezi Disemba  kwa dau la milioni 30 za Kitanzania, huku akiahidiwa kupewa nyumba ya kuishi.

Mchezaji huyo ( Kessy) hivi sasa amekosa furaha baada ya kucheza kwa miezi mitatu pasipo kumaliziwa pesa yake inayofikia milioni Kumi, huku akiishi kwa kuhama hama. Kessy amekuwa akiishi katika makazi ya wachezaji wenzake kitendo ambacho kinamfanya kukosa uhuru.
“ Sitarejea kikosini hadi nitakapotimiziwa mahitaji yangu yaliyopo katika mkataba” anasema mchezaji huyo wakati nipozungumza naye muda mfupi uliopita akiwa Mkoani Morogoro. Simba ilikubali kumlipa mchezaji huyo kiasi cha milioni 30 na kumpatia milioni 20 huku wakimuhakikishia kuwa ndani ya miezi mitatu-Disemba-Machi watamkamilishia kiasi kilichobaki pamoja na kumpatia nyumba.
“ Walinihakikishia kuwa ndani ya miezi mitatu watakuwa wamekamilisha kila kitu” anaendelea kusema mchezaji huyo aliyeingia moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Simba. Timu hiyo itacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga mwishoni mwa wiki hii kupitia msemaji wake, Hajji Manara imekanusha vikali madai ya mchezaji huyo na kudai kuwa yuko nje ya timu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia, jambo ambalo Kessy amelikataa na kusisitiza kuwa ‘ matatizo ya kimkataba ndiyo yaliyomuondoa’.
Hii si mara ya kwanza kwa wachezaji wa Simba kugoma, ikumbukwe kuwa msimu wa mwaka 2010/11 timu hiyo ilimsaini mshambulizi Mbwana Samatta kutoka African Lyon na kumuahidi kumpatia gari lakini mara baada ya Samatta ( wakati huo akiwa na miaka 18) kusaini alianza kuzungushwa hadi kufikia hatua ya mchezaji kugomea kujiunga na timu hiyo.samatta smba
Samatta alikosa michezo yote ya mzunguko wa kwanza na alipopewa gari lake alirudi uwanjani kwa kasi na kufunga mabao Nane katika michezo ya mzungoko wa Pili kabla ya kuuzwa kwa TP Mazembe ya DR Congo mwishoni mwa msimu kwa ada ya milioni 150. Kama kweli nia ya uongozi ni kuifanya timu hiyo kurejea katika kiwango cha juu bila shaka wanatakiwa kuwa makini zaidi na kutatua haraka matatizo kama haya ya Kessy ambayo yako ndani ya uwezo wao.
Naamini suala la Kessy kwa kiasi Fulani litakuwa linawachanga watu wa benchi la ufundi na hata uongozi kiujumla ingawa walikuwa na nafasi kubwa ya kumalizana na mchezaji huyo ni kama utawala umepuuzia hivyo mchezaji ameamua kufanya kitu kama ‘ kujitoa sadaka’. Upande mwingine naamini mchezaji huyo amefanya haraka, Kessy amechukua uamuzi wa kuondoka kwa muda kikosini siku ya mwisho ambayo aliahidiwa kulipwa, labda ni kwa nia ya kusisitiza kuhusu msimamo wake na je, ni kwanini uongozi umeshindwa kuzungumza na mchezaji huyo hadi amefikia hatua ya kujitoa kambini?
-MATUKIOTZ

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA