Wednesday, 22 April 2015

KWELI MPIRA UNADUNDA.!!BAYERN YAAMKA, YAICHAPA FC PORTO 6-1, YASONGA KWA BAO 7-4

Ikicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena jijini Munich, timu soka ya Bayern Munich imeifanyia mauaji ya kutisha FC Porto baada ya kuitngua kwa jumla ya mabao 6-1 katika mchezo ambao wenyeji hao walicheza kufa na kupona kuhakikisha wanasonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa awali wa robo fainali uliochezwa Lisbon, Ureno wiki iliyopita, Bayern Munich usiku wa kuamkia leo walijifunga mkwiji na kuonyesha soka la kijerumani la kufia uwanjani na kufanikiwa kupata mabao 6-1 hivyo kuiweka Porto pembeni nao kuingia nusu fainali. 

Mabao ya Bayern yaliwekwa kimiani na Thiago Alcantara katika dakika ya 14, Jerome Boateng akifunga bao la pili katika dakika ya 22, nae Robert Lewnadowski akifunga mabao mawili katika dakika za 27 na 40.

Bao la tano lilifungwa na Thomas Muller kunako dakika ya 36 na bao la sita nala ushindi lilifungwa na Xabi Alonso katika dakika ya 88.
Wachezaji wa Bayern Munich wakiwa mbele ya mashabiki wao baada ya kumalizika kwa mchezo huo. Kwa matokeo hayo, Bayern imesonga mbele kwa jumla ya mabao 7-4







0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA