Wednesday, 22 April 2015

NEYMAR AIZAMISHA PSG WAKATI FC BARCELONA IKISONGA MBELE HATUA YA NUSU FAINALI YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA

Beki wa FC Barcelona, Dani Alves akiwa amembeba mshambuliaji wao Neymar baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Paris Saint Germain usiku wa kuamkia leo katika uwanja wa Nou Camp jijini Barcelona, Hispania.
Timu ya soka ya FC Barcelona usiku wa kuamkia leo imesonga mbele kwa kishindo katika hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuitandika Paris Saint Germani ( PSG ) mabao 2-0 katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani humo. 

Alikuwa ni mshambuliaji Neymar raia wa Brazil aliyeipeleka nusu fainali Barcelona baada ya kufunga mabao yote mawili katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Nou Camp, jijini Barcelona nchini Hispania. 

Neyamar alifunga bao la kwanza katika dakika ya 14 na kisha akafunga bao la pili nala ushindi katika dakika ya 34. 

Kwa matokeo hayo, Barcelona imesonga mbele kwa idadi ya magoli 5-1. Katika mchezo wa awali, Barcelona waliifunga PSG mabao 3-1 jijini Paris.






0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA