Tuesday, 21 April 2015

LIGI YA MABINGWA ULAYA, PSG KUJIULIZA KWA BARCELONA NAO BAYERN KUSUKA AU KUNYOA KWA PORTO LEO USIKU


Eeeh Mungu nisaidie mie Guardiola nishinde leo!! Kocha mkuu wa Bayern Munich, Pep Guardiola akifuatilia mazoezi ya wachezaji wake huku akiwa mwenye mawazo. Anatakiwa kushindi mchezo wa leo baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa awali.
Wachezaji wa Paris Saint Germain ( PSG ) wakijifua katika uwanja wa Nou Camp jijini Barcelona nchini Hispania kabla ya mchezo wao wa marudiano na FC Barcelona leo usiku.

Ligi ya mabingwa barani Ulaya michezo ya marudiano robo fainali ya ligi hiyo itachezwa leo usiku katika viwanja viwili tofauti. Bayern Munich ambayo inasumbuliwa kwa kuwa na majeruhi, watakuwa nyumbani katika uwanja wa Allianz Arena kucheza na FC Porto toka Ureno. 

Katika mchezo wa awali, Porto waliifunga Bayern mabao 3-1 na kujiweka pazuri katika mchezo wa leo kusonga mbele hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo. 

Wenyewe FC Barcelona ambao nao watakuwa katika uwanja wa nyumbani, wana nafasi nzuri ya kutinga hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo baada ya mchezo wa awali kuwafunga PSG nyumbani kwao mabao 3-1. 

PSG wamejiandaa vyema kwa mchezo wa leo na wanamtegemea sana mshambuliaji wao Zlatan Ibrahimovic ambaye mchezo wa awali hakuwemo na Marco Verratti. Wawili hawa walikuwa na kadi za njano ndio maana walikosa mchezo wa awali mjini Paris, Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA