Tuesday, 21 April 2015

WASTARA APATA AJALI TENA TABATA JIJINI DAR

Wastara baada ya kupata ajali.
MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma jana amepata tena ajali wakati akielekea nyumbani kwake maeneo ya  Tabata-Bima jijini Dar es Salaam.
Wastara alijigonga katika kioo cha mbele cha gari lake baada ya kutaka kuvaana na gari kubwa na kulazimika kufunga breki za ghafla akiwa hajafunga mkanda. Msanii huyo ameumia sehemu za usoni.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wastara aliandika hivi:
"DUA ZENU MUHIMU SANA KWA MBAO MNAONIPENDA NA MSIONIPENDA......hali hii imenichosha sana ya matukio ya ajali kila mara natamani kuwa na amani na maisha yangu couz mungu ana sababu kuniacha niendelee kupumua mpka leo ila kwa wanaochukia kuona napumua wanatamani nizikwe hta mzima ila mtambue nina watot 3 wananitegemea kwa kila kitu smtime mnasema nasikitika sana ni kweli sababu mi sio nabii nikihesabu hii ni ajali ya ya 9 sasa tena ni mbaya sana za kufa kabsa ila labda nimo kwa wale wanaopta ajali kipindi hiki japo kwangu ni too much,, ni jana na leo napumua alhamdulilah duwa zenu niombeni jamani huyu jinamizi akae mbali nami daah too much"
Wastara ameshapata ajali mara kadhaa ikiwemo ile ya mwaka jana wakati akitoka nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar na gari lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili ya kwenda kununua umeme pamoja na ile ya pikipiki aliyopata mwaka 2008 akiwa na aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi akatwe mguu wa kulia. Pia aliwahi kupata nyingine ya gari akiwa na Sajuki.
Mtandao huu unampa pole msanii huyo na kumtia moyo katika shughuli zake.
CREDIT GPL & INSTAGRAM

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA