ARSENAL YAFIA EMIRATES,YACHAPWA NA SWANSEA 1 BILA
Bafetimbi Gomis akiipatia Swansea City goli pekee na la ushindi |
Timu ya soka ya Arsenal imeshindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani(Emirates Stadium) baada ya kuchapwa bao moja kwa bila na Swansea City katika mchezo wa ligi kuu Uingereza uliopigwa Jumatatu usiku.
Arsenal iliyokuwa inataka kulipa kisasi kwa Swansea baada ya kufungwa katika mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Novemba mwaka jana ilijikuta katika wakati mgumu kwa kushindwa kumfunga mlinda mlango wa zamani wa timu hiyo Lukasz Fabianski aliyekuwa imara na kuchomoa mashuti yaliyolenga langoni mwake.
Zikiwa zimesalia dakika tano kwa mechi kumalizika,Gomis ambaye katika msimuu huu amepeleka msiba mara mbili kwa Arsenal ikikumbukwa kuwa ndiye aliyepachika bao la ushindi wakati Swansea ikiilaza Arsenal mwaka jana,kwa mara nyingine akiingia toka benchi kuchukua nafasi ya Ki Sung-yueng alitumia vyema kichwa chake kufunga bao ambalo ilibidi lihitaji utaalam wa Goal Line Technology na referee kulikubali.
Ushindi huu unaifanya Swansea City kuweka rekodi ya kuifunga Arsenal nje ndani katika ligi kuu kwa mara ya pili tangu walipofanya hivyo msimu wa 1981-82.
Mbele ya mashabiki 59,989 Arsenal imejikuta ikizuiwa kuifikia Manchester City yenye alama 73 na kusalia na alama 70 ikiwa ni alama mbili pekee mbele ya Manchester United huku ikiwa na kibarua cha kuelekea Old Trafod kuwakabili mashetani hao wekundu.
Picha na BBC SPORT
0 comments:
Post a Comment