Wednesday 13 May 2015

FC BARCELONA HIYOOO..YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA KWA JUMLA YA MABAO 5-3


HATIMAYE BAYERN OUT!! Timu ya soka ya Bayern Munich ya Ujerumani usiku wa kuamkia leo wameshuhudia wakishindwa kufuzu kucheza fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kujikuta wakiondolewa na FC Barcelona kwa jumla ya mababo 5-3. 

Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena uliofurika mashabiki wenye pumzi ya kushangilia bila kuchoka, Bayern waliokuwa na kibarua cha kuifunga Barcelona mabao 4-0 ili wasonge mbele hatua ya fainali, walijikuta wakimaliza dakika 90 za mchezo huo wakiwa na ushindi wa magoli 3-2 ambayo hayakutosha kuwavusha. 

Mabao ya Bayern yaliwekwa kimiani na Medhi Benatia dakika ya 7, Robert Lewandowski dakika ya 59 na Thomas Muller aliyefunga bao la tatu katika dakika ya 74. 

Mabao mawili ya FC Barcelona yalifungwa na Neymar katika dakika za 15 na 29 

Ushindi huo wa mabao 3-2 haukutosha kuwavusha Bayern Munich, kwani katika mchezo wa awali uliochezwa Camp Nou, Wajerumani hao walifungwa mabao 3-0. 

Kwa idadi hiyo ya mabao ilikuwa ni faida kubwa kwa Barcelona kuchomoza fainali kwa jumla ya mabao 5-3. 

Sasa wanasubiri kucheza fainali na mshindi wa mchezo mwingine wa leo marudiano wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid ambao ni mabingwa watetezi watakaokuwa wanacheza na Juventus ya Italia.
Aaah wewe dogo ni mkali, nimekukubali!!! Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola akimpa mkono mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi mara baada ya mchezo huo.
Gerard Pique akikwaana na starika wa Bayern, Robert Lewandowski, aliyekuwa amevaa mask baada ya kuvunjika pua yake.



0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA