Thursday 14 May 2015

REAL MADRID YAVULIWA UBINGWA WA UEFA NYUMBANI,MORATA AIPELEKA JUVENTUS FAINALI

Mabingwa watetezi wa kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya, timu ya soka ya Real Madrid ya Hispania usiku wa kuamkia leo wamevuliwa ubingwa huo na bibi kizee cha Turin, Juventus ya Italia baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1. 

Katika mchezo huo wa marudiano wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, Juventus imesonga mbele kwa idadi ya mabao 3-2. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Italia, Juventus iliifunga Real Madrid magoli 2-1.
Katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo, Madrid wakicheza mbele ya maelfu ya mashabiki wao walijitahidi kulisakama lango la wapinzani wao lakini uimara wa kipa mkongwe wa Juventus, Buffon uliwanyima nafasi nyingi za kufunga goli. 

Bao lao lilipatikana kwa mkwaju wa penati uliofungwa na Cristiano Ronaldo katika dakika ya 23, bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. 

Kipindi cha pili Juventus walikuja juu na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Alvaro Morata kunako dakika ya 57.
Kwa matokeo hayo, Real Madrid waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo wamevuliwa ubingwa huo, na sasa fainali itazikutanisha FC Barcelona ya Hispania na Juventus ya Italia. Mchezo wa fainali utachezwa June 06' 2015 mjini Berlin, nchini Ujerumani.
TUNAWASHUKU SANA, TUKUTANE BERLIN!! Wachezaji wa Juventus wakiwashukuru mashabiki wao baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Real Madrid.



0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA