Friday 26 June 2015

UBINGWA WAZIDI KUNUKIA NYUMBANI,,CHILE YAICHAPA URUGUAY NA KUTINGA NUSU FAINALI COPA AMERICA

Timu ya Taifa ya Chile imetinga nusu fainali ya michuano ya mataifa ya America kusini (Copa America) baada ya kuitandika Uruguay goli 1-0 katika mechi ya robo fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa Santiago.
Goli pekee la wenyeji Chile lilifungwa na Mauricio Isla katika dakika ya 81'.
Dakika ya 63' Uruguay ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake Edinson Cavani kuoneshwa kadi nyekundu kufuatia kuoneshwa kadi ya kwanza ya njano kwa kosa la kumtukana mwamuzi wa mechi.
Wakati huo huo beki Jorge Fucile naye alioneshwa kadi ya pili ya njano na hatimaye nyekundu katika dakika ya 90' baada ya kumchezea vibaya Alexis Sanchez wa Chile.
Kwa matokeo hayo, Chile itacheza nusu fainali dhidi ya mshindi wa mechi ya robo fainali itakayowakutanisha Bolivia na Peru.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA