OKWI RASMI DENMARK MIAKA MINNE
14:13 |
No Comments |
Klabu ya Sonderjyske inayoshiriki ligi kuu ya Denmark (ALKA Superliga) imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi kwa mkataba wa kudumu wa miaka minne na ametambulishwa rasmi.
Okwi, raia wa Uganda amepewa jezi namba 25 ambayo alikuwa anaivaa akikipiga Simba .Okwi hajafanya majaribio katika klabu hiyo kama walivyodai Simba bali amesaini moja kwa moja na siku chache zijazo ataanza kucheza mechi za ligi kuu.
Mtandao rasmi wa klabu ya Okwi umethibitisha kumsajili
MAELEZO MAFUPI YA TIMU MPYA YA OKWI
SønderjyskE ni shirika la michezo la Denmark linalomiliki timu ya mpira wa miguu inayoitwa SønderjyskE Fodbold, yenye makazi yake mjini Haderslev.
Pia linamiliki timu mbili za mpira wa mikono, SønderjyskE Håndbold, moja ya wanaume yenye masikani yake mjini Sønderborg, moja ya wanawake inayokaa mjini Aabenraa.
Pia lina timu ya ice hockey ijulikanayo kwa jina la SønderjyskE Ishockey, yenye makazi yake mjini Vojens.
Timu zote hizi zinacheza ligi za kaskazini mwa Jutland inayojulikana kwa jina la Sønderjysk Elitesport (Kwa kiingereza: Southern Jutlandic Elite Sport).
SønderjyskE ni timu iliyoundwa kwa ajili ya Jimbo zima la Jutland kaskazini kwa lengo la kuleta ushindani katika ligi za juu za Denmark na timu hii iliweka maskani yake mjini Haderslev ikiitwa Haderslev FK.
Mwaka 2004, timu zote, yaani ya mpira wa miguu, ice hockey na handball chini ya Shirika hilo la SønderjyskE, zilianza kuwakilisha ukanda mzima wa Jutland Kaskazini na sio mji mmoja tena. Zilivuta hisia za watu, wadhamini, mashabiki na vyombo vya habari kutokana na kuchukua vijana wengi wenye vipaji .
Kwasasa timu 5 zinacheza katika ligi bora za Denmark, huku timu ya mpira wa miguu ikiwa tishio katika ligi kuu ya Denmark.
Hizi ndizo timu zinazoshiriki ligi kuu ya Denmark kwa msimu wa 2015/2016
Matokeo ya mechi za karibuni za timu ya Okwi na ratiba ijayo…
Related Posts:
HAPANA CHEZEA KIFO:::FISI AJIFICHA NDANI YA MZOGA KUYAOKOA MAISHA YAKEHabari Mdau wa Funguka Live ,leo nimeona tujikumbushe kisa hiki cha kusisimua sana ambapo ni nadra sana kupatikana , nimatumaini yangu utafurahi na ku… Read More
PICHA::WAZIRI MKUU WA INDIA ALIPOWASILI NCHINI Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi akipunga mkono kusalimia wananchi waliojitokeza kumlaki mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege … Read More
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA MRADI WA GREEN VOICES TANZANIA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa na kinyago cha mwanamke baada ya kuzindua mradi wa Green … Read More
EXCLUSIVE TIPS:; MWANAMKE AKIKUJIBU HIVI KAMA UNACHAT NAE ACHA KABISA....!! Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsal… Read More
MNYIKA AKANUSHA UVUMI UNAONDELEA KATIKA MITANDAO, AELEZA MSIMAMO WAKE NDANI YA CHAMA Picha toka maktaba/ Mwananchi Baada ya kuenea kwa uvumi kuwa Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika anataka kuachana na chama hicho, kiongozi h… Read More
0 comments:
Post a Comment