Monday 10 August 2015

MWENYEKITI WA CCM ARUSHA ATIMKIA CHADEMA


Aliyekuwa Kigogo wa Chama cha Mapinduzi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Mh Onesmo Nangole na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isack Joseph wamejiuzulu nafasi zao zote na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Wakizungumza mara baada ya kutua Upinzani vigogo hao wamemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kuacha mara moja siasa za matusi za kuwaita Makapi wanachama ambao wamekuwa wakijiunga na vyama vya upinzani.
Licha ya Vigogo hao kuhamia chadema wanachama wengine zaidi ya mia 300 waliokuwa chama cha CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli juzi walizichoma kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA .
Katika hatua nyingine Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye amedai kwamba kumekuwepo na hujuma zinazofanywa na upinzani kwa kuchapisha kadi feki za CCM kisha kupewa wananchi ili waonekane kama kweli wanakihama chama hicho.
Kwa upande wa uongozi wa juu wa Chadema umewataka wananchi wote wanao choshwa na Siasa za CCM kuhamia chama hicho kwa kuwa kila mwananchi ana uhuru wa kuhamia chama chochote cha Siasa anachokipenda.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA