Sunday 6 September 2015

TAIFA STARS ILIVYOCHUANA NA NIGERIA


Basi lililobeba wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars likiingia lango kuu la Uwanja wa Taifa
 
 
 
Basi lililobeba wachezaji na viongozi wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles pamoja na msafara wa mashabiki wa timu hiyo ukiingia katika lango kuu la Uwanja wa Taifa

Picha na Dickson Mulashani (http://www.fungukalive.com/)
KIKOSI cha timu ya soka taifa Tanzania ‘Taifa Stars’  kimelazimishwa sare ya bila kufungana na kikosi cha timu ya taifa Nigeria ‘Super Eagle’, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo wa kufuzu Mataifa, umeifanya Stars, kujipatia pointi moja katika kundi lake D lenye timu za Chad, Misri na Nigeria.
Timu hizo zilianza mchezo kwa kasi na dakika ya tatu ya mchezo nahodha wa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, akishinda kuunganisha vyema mpira wa kona uliochongwa na Farid Mussa.
Dakika ya 10, mshambuliaji wa Nigeria Emmanuel Emenike, alishindwa kuunganisha mpira wa kichwa uliochongwa na Mosses Simon, ambaye alimpa wakati mgumu beki wa Stars, Shomari Kapombe.
 

Mashabiki wa timu ya taifa ya Tanzania wakionesha ishara ya magoli kwa vidole


Mashabiki wa Nigeria wakihanikiza timu yao


Stars, ilijibu shambulizi hilo dakika ya 13 baada ya wachezaji wake Mussa na Mbwana Samatta kugongeana vyema na Samatta kupiga shuti hafifu, lililodakwa na kipa wa Nigeria Ikeme Onora.
Dakika mbili baadaye Samatta, alipiga kichwa akipokea pasi ya Thomas Ulimwengu, lakini hata hivyo kichwa hiko hakikuwa na nguvu na kufanya mabeki wa Nigeria waondoe hatari hiyo langoni mwao.
Dakika ya 36 Simon wa Nigeria, alishindwa kuipatia bao timu yake baada ya safu ya ulinzi ya Stars, kujichanganya yenyewe katika kuokoa.
Mpaka mchezo huo unakwenda mapumziko timu hizo zilishambuliana kwa zamu bila kufungana bao, huku mshambuliaji wa Nigeria, Emenike akiwa mwiba mchingu kwa safu ya ulinzi ya Stars.
Mchezo huo ulirudi kipindi cha pili na timu hizo zikaendelea kushambuliana kwa zamu, huku kila upande ukikosa nafasi za kufunga mabao.
 Makocha wa timu zote walifanya mabadiliko kadhaa ya kuwatoa baadhi ya wachezaji wao, lakini milango ya timu zote iliendelea kuwa migumu.
Stars: Ally Mustapha ‘Barthez’, Kapombe, Hajji Mwinyi Mgwali, Haroub, Kelvin Yondani, Himid Mao, Mrisho Ngasa / John Bocco ‘Adebayor’, Mudathir Yahaya / Said Hamis ‘Ndemla’, Samatta na Ulimwengu.
Nigeria: Onora, Solomon Kwambe, Kingsley Madu, Keneth Omeruo, William Ekong, Nwankwo Obiora, Ahmed Mussa, Haruna Lukman / Igboun Emekea, Emenike / Ujah Anyhony, Uzochukwu Izzuna na Simon / Edouk Samuel.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA