Monday, 9 November 2015

Taarifa ya Polisi Mbeya: Wachina wakamatwa na pembe 11 za faru



JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA RAIA WANNE WA NCHINI CHINA WAKIWA NA PEMBE 11 ZINAZODHANIWA ZA FARU.

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE RAIA WA CHINA WAKIWA NA PEMBE 11 ZINAZODHANIWA ZA FARU. RAIA HAO WALIFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. XIAO SHAODAN (29) AKIWA NA PASSPORT NAMBA G.29624553 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA 2. CHEN JIANLIN (33) AKIWA NA PASSPORT NAMBA E.09800855 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA 3. SONG LEI (30) AKIWA NA PASSPORT NAMBA G.52064944 ILIYOTOLEWA NCHINI CHINA NA 4. HU LIANG (30) WOTE WAKAZI WA BLANTYRE NCHINI MALAWI.

WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 06.11.2015 MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO MPAKANI KASUMULU KATIKA WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA BAADA YA ASKARI POLISI NA WADAU WENGINE WA USALAMA WALIOKUWEPO MPAKANI HAPO KULITILIA MASHAKA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.103 DER AINA YA TOYOTA HILUX RANGI YA DHAHABU LILILOKUWA LIKITOKEA NCHI MALAWI KUINGIA TANZANIA LIKIWA NA RAIA HAO.


KUTOKANA NA MASHAKA HAYO, MAAFISA HAO WALIFANYA UPEKUZI NDANI YA GARI HILO NA CHINI YA CHASES YA GARI HILO NA NDIPO WALIGUNDUA KUWA GARI HILO LILIKUWA LIMEJENGEWA BOKSI NA BAADA YA KUFUNGUA BOKSI HILO LA BATI KULIPATIKANA PEMBE 11 ZA MNYAMA PORI FARU.

AIDHA ASKARI POLISI WALIENDELEA NA UPEKUZI KATIKA GARI HILO NA KUKUTA MALI MBALIMBALI ZIKIWEMO:- SIMU MOJA AINA YA SAMSUNG, IPAD MOJA, PESA YA MALAWI KWACHA 1,600/=, TSHS.234,000/=, USD DOLLAR 1,700/=, NOTI 22 @ TSHS 100 = 2,200, NOTI 51 @ TSHS 51 = 2,550, USD 33 @ TSHS. 50 = 1,650, USD NOTI 9 @ TSHS 100 = USD 900, MALAWI KWACHA 18,760 NA CERTIFICATE OF HEALTH EXAMINATION MOJA, SIMU MBILI ZA KICHINA AMBAZO MAJINA YAKE NA AINA HAIKUFAHAMIKA MAPEMA NA SIMU MOJA AINA YA HUAWEI, SIMU MOJA AINA YA SAMSUNG, IPHONE APPLE TANO, SIMU MOJA TARDROVER, NOKIA MOJA NA SMT MOJA.
UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILI UNAENDELEA NA PINDI UTAKAPOKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA FARU/PEMBE ZA NDOVU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA PEMBE ZA FARU/NDOVU KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA