BODI YA MIKOPO YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOENEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU KUTOTOA MIKOPO KWA WAOMBAJI WENYE SIFA
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA
2015/2016
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuutaarifu umma kuwa kuna
taarifa zinazosambazwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa
mikopo kwa waombaji wapya kwa mwaka wa masomo 2015/2016. Taarifa hizo si za
kweli na hivyo Bodi inauomba umma kuzipuuza.
Aidha,
Bodi ya Mikopo inapenda kutoa taarifa kwamba hadi sasa imekwishawapangia mikopo
jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 40,836
wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya
waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata
mikopo na katika Awamu ya Pili iliyotolewa tarehe 9 Novemba, 2015 jumla ya waombaji
28,554 wamepangiwa mikopo.
Majina
ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili
yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz
na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo
pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Lengo
la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa kupata
mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016, ambao ni 50,830, wanapata mikopo.
Aidha,
Bodi inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu wakati mchakato wa
upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa unaendelea.
Imetolewa
na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA
MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
0 comments:
Post a Comment