Saturday 19 December 2015

CHEKI "BEHIND THE SCENE" YA UTAIPENDA WA DIAMOND


                            Diamond akipiga kinanda huku akimuimbia mpenzi wake Zari.
                                                                                     Diamond akiongea jambo.
Sasa hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda.

Ni ngoma kali ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar.

Mbali na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo, nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB).

Itakuwa ni siku ya Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii wengine kibao.

Burudani yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000.

Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo kikiandaliwa.

Video hiyo ni mkono wa yuleyule mkali wa vichupa kutoa Sauzi anayekwenda kwa jina la God Father. Hajakosea! Amefanya bonge la kazi na hata mashabiki ni mashahidi kwamba wimbo ni mkali na kideo chenyewe ni ‘kitamu’.

Maneno mengi siyo ishu, kwenye hili picha zinaongea zaidi hivyo pitisha macho kwenye baadhi ya picha hizo ili upate uhondo!
Kwani kuna mtu kaibiwa?

<strong>Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

0 comments:

Post a Comment

OFFICIAL MEMBER

OFFICIAL MEMBER

Please Share This Site

HABARI ZETU

LIKE PAGE YETU HAPA