CHELSEA "MBOVU" YA EPL YASONGA MBELE UEFA
Chelsea imefuzu hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibugiza FC Porto kwa mabao 2-0.
Ushindi huo umevusha Chelsea kwa uhakika zaidi kwa kuwa kinara wa Kundi G ikiwa na pointi 13 na kufuatiwa na Dynamo Kiev ambayo imeishinda Maccabi 1-0 leo na kufikisha pointi 11, hivyo kuindoa Porto yenye pointi 10.
Shukurani kwa bao la kujifunga kwa Porto, lakini shukurani zaidi kwa William ambaye alifunga bao kwa shuti kali ile mbaya baada ya Oscar na Diego Costa kugongeana mpira kwa haraka.
0 comments:
Post a Comment