LIVERPOOL YAFUZU "32 BORA" EUROPA,YAUNGANA NA MACHESTER UNITED
TIMU ya Liverpool imewafuata mahasimu, Manchester United katika 32 Bora ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kulazimisha sare ya 0-0 ugenini jana na FC Sion katika mchezo wa mwisho wa Kundi B wa michuano hiyo Uwanja wa Tourbillon. Liverpool sasa inamaliza kileleni mwa kundi hilo, baada ya kutimiza pointi 10, mbele ya FC Sion iliyomaliza na pointi tisa. Mchezo mwingine wa kundi hilo, Bordeaux imelazimishwa sare ya 2-2 na Rubin Kazan Uwanja wa Matmut Atlantique, hivyo kupoteza nafasi ya kusonga mbele.
Ikumbukwe Manchester United imeangukia katika Europa League baada ya kutolea katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA.
Sasa timu hizo zitasubiri droo itakayochezeshwa siku ya jumatatu ili kujua nani anamkabili nani katika hatua ya 32 bora.
0 comments:
Post a Comment